• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SENYAMULE AZINDUA MPANGO MKAKATI WA KUZIBITI MIGOGORO YA ARDHI

Imetumwa : July 18th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ametoa wito kwa Halmashauri ya jiji la Dodoma na kamati ya ardhi kufanya kazi kwa weledi ili kuutendea haki Mpango Mkakati wa kutokomeza kero za migogoro ya ardhi ambayo imekuwa mwiba mchungu kwa wananchi na kuchafua taswira ya jiji hilo kwa muda mrefu.

Wito huo umetolewa leo Julai 18,2023 wakati akizindua Mpango Mkakati wa Mkoa wa kushughulikia migogoro ya ardhi katika jiji la Dodoma halfa iliyohudhuriwa pia na Watumishi wa Halmashauri ya Jiji hilo, Madiwani, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na Mkoa na Kamati ya Amani yenye wajumbe kutoka (dini mbambali) na vyombo vya habari.

"Kwa muda mrefu Mamlaka mbalimbali za Serikali zimekuwa zikijitahidi kutatua migogoro hii lakini imekuwa haiishi na wananchi kuendelea kulalamikia Serikali. Kwa uchunguzi tuliofanya kama mkoa tulibaini malalamiko mengi ni ya fidia na watu walioahidiwa kupewa viwanja mbadala. Kimsingi maelekezo mbalimbali yalikuwa yanatolewa ili kutafuta ufumbuzi wa suala hili.

"Napenda kuujulisha umma huu kuwa tarehe 27/06/2023 niliunda Kamati Maalumu ya kushughulikia tatizo hili na mnamo tarehe 7/7/2023 Kamati imewasilisha Mkakati huo ambao pamoja na hatua nyingine kama Mkoa tumejipanga kuutekeleza ili kutatua migogoro ya ardhi Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akiagiza kusikiliza kero za wananchi na kutoa ufumbuzi lakini pia dhamira ya kutaka kuona Jiji la Dodoma linakuwa Jiji bora na lenye hadhi"ameeleza Senyamule

Pia, Mhe. Senyamule amesema mkakati huo wa muda mfupi na muda mrefu utaenda kuhakikisha migogoro katika jiji la Dodoma inamalizika na kuwafanya wananchi wa Dodoma kuishi kwa Amani, utulivu na kuepuka migogoro isiyo ya lazima.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa Uongozi wa Jiji wamejipanga vizuri katika kuhakikisha wanatatua changamoto za ardhi zilizopo kupitia Mkakati huo uliopangwa kutekelezwa kwa muda wa mwaka mmoja ambao unaanzia julai 2023 na unatarajiwa kukamilika ifikapo juni 2024.

‘’Nikuhakikishie Mhe. Mkuu wa Mkoa mimi na timu yangu tumejipanga vizuri kutekeleza Mkakati huu tutafanya vizuri kwasababu tumepanga kutoka ndani yetu kwahiyo kwa kujiamini tutasimamia na tutakuwa wakali kwa wote watakaotaka kutukwamwisha katika zoezi hili" Amesema Shekimweri

Kwaupande wake Kamishna wa

Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dodoma Jabir Singano amesema katika kuhakikisha changamoto hizo zinatatuliwa wataendelea kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na watahakikisha wanaongeza idadi ya watumishi wa ardhi ili kuongeza nguvu kazi ya kutatua kero hizo.

Katika kikao hicho Senyamule amezitaja changamoto zitakazopatiwa ufumbuzi ni pamoja na Madai ya viwanja mbadala, Madai ya fidia, Madai ya upimaji shirikishi wa 70% kwa 30%, Uvamizi wa viwanja, ucheleweshaji wa Hati miliki, ukosefu wa huduma bora kwa wananchi, Miliki pandikizi na mabadiliko katika Usimamizi wa Sekta ya Ardhi.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.