• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI IMESHAFANYA MAMBO MAKUBWA KUTUWEZESHA KUINUKA-RC SENYAMULE

Imetumwa : March 5th, 2025

Na Francisca Mselemu

      Dodoma RS

Kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Rosemary Senyamule amewataka wanawake  wa Mkoa huu kutokusita kufanya biashara kubwa kwa sababu uwezo wanao, na tayari Serikali imeshaweka mazingira wezeshi.

Mheshiwa Senyamule ameyasema hayo leo Februari 05,2025 wakati wa Kongamano la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi lililoandaliwa na Taasisi ya ‘The Tunu Pinda Foundation kwa kushirikiana na Taasisi ya ‘Tanzania,China Women Empowerment Foundation’ na kufanyika katika Ukumbi wa Vijana Social Hall uliopo Area C Jijini Dodoma, ambapo alikuwa Mgeni Rasmi.


Akizungumza wakati wa hotuba yake, Mheshimiwa Senyamule amesema ‘‘Mara nyingi  Wanawake tumezoea kufanya biashara ndogondogo, zinazofanana fanana, tujiingize kwenye biashara kubwa kwa sababu uwezo tunao,na Serikali Yetu imeshafanya mambo makubwa kutuwezesha kuinuka”.

Aidha, Mhe. Senyamule amempongeza mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bibi Tunu Pinda(Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu) kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuhudumia Jamii, ambapo amesema kuwa Taasisi hiyo ilianza kwa udogo,lakini kutokana na upendo na matamanio yake ya kuona watu wanapiga hatua, na kwa sababu ya dhamira ya dhati aliyokuwa nayo, ndani ya muda mfupi imeweza kufanya mambo makubwa.


Kadhalika, Mhe. Senyamule amesema kuwa pamoja na kujivunia mafanikio makubwa ya wanawake katika miaka 30 ya Beijing, wanawake hao wanapaswa kutambua mchango wa wanaume.


‘’Tunaposhuhudia na kufurahia uwepo wa Rais Mwanamke, ni muhimu kufahamu kuwa hakuingia mwenyewe kwenye hiyo nafasi, bali alikuwepo Kiongozi mmoja ambaye katika historia ya Nchi Yetu ni Kiongozi wa kwanza kumteua Makamu wa Rais Mwanamke, na ndiye huyu Rais wetu Samia Suluhu Hassan, ambaye ameonesha uwezo na kipaji kikubwa kilichopo ndani yake.


Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, ambaye pia ni mlezi wa Taasisi hiyo amesisitiza juu ya umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii.

“Uwe mwanaume,au mwanamke,ni lazima ukubali kwamba ili maisha yako yawe bora  ni lazima uchumi wako ubadilike,na ili uchumi ubadilike, ni lazima ufanye kazi , tena kwa bidi, ubunifu wa hali ya juu,na kutokuchagua kazi ”Amesema Mhe. Pinda.


Kongamano hilo lilikwenda sambamba na kukabidhi mabegi ya shule kwa ajili ya Wanafunzi wa shule mbalimbali za Dodoma pamoja na vyerehani kwa baadhi ya Wanawake na Viongozi wa Gereza la Isanga ili Wafungwa Wanawake waliopo katika gereza hilo waweze kufundishwa ushonaji, watakapomaliza kutumikia vifungo vyao wawe na ujuzi utakaowawezesha kukuza uchumi wao ambapo vitu hivyo vimetolewa na Taasisi hizo.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.