• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI IMETENGA BIL.9.9 UJENZI WA VITUO SABA VYA ZIMAMOTO NA UOKOAJI - MAJALIWA

Imetumwa : April 26th, 2023

SERIKALI IMETENGA BIL. 9.9 UJENZI WA VITUO SABA VYA ZIMAMOTO NA UOKOAJI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga shilingi bilioni 9.93 katika bajeti ya mwaka 2023/2024 kwa ajili ya kukamilisha miradi ya ujenzi wa vituo saba vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Amesema kuwa vituo hivyo vitajengwa katika Mikoa ya Songwe, Simiyu, Kagera, Njombe, Manyara, Katavi na Geita.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano (Aprili 26, 2023) wakati akifungua vituo vya kisasa vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji vya Nzuguni na Chamwino mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya miradi inayozinduliwa katika juma la kilele cha maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Vituo hivyo vimegharimu zaidi ya shilingi bilioni 2.3.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa ujenzi wa vituo hivyo pamoja na upatikanaji wa vitendea kazi vya kutosha vitasaidia kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao unakuwepo.

“Kukamilika kwa miradi hii kutasaidia kusogeza huduma za zimamoto na uokoaji karibu zaidi na wananchi na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma za zimamoto na uokoaji kwa kufika eneo la tukio kwa wakati”

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa miradi mingine inayotekelezwa na Serikali ni ujenzi wa Ofisi ya Kisasa za Jeshi la Zimamoto Temeke, Dar es Salaam, vituo vya polisi vya daraja A vya Kigamboni Dar es Salaam na Wanging’ombe Mkoani Njombe.

Mingine ni Ofisi za Uhamiaji za mikoa ya Lindi na Geita na Ofisi za Makamanda wa Polisi katika Mikoa ya Kusini Unguja na Kaskazini Unguja. “Miradi hiyo yote imegharimu zaidi ya shilingi bilioni 16”.

Ameongeza kuwa, Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kutekeleza dhamira yake ya kufanya maboresho makubwa na ya kiutendaji pamoja na ujenzi wa miundombinu muhimu ya Jeshi la Zimamoto yenye lengo la kuimarisha ufanisi katika utendaji wa jeshi hilo.

Aidha, Waziri Mkuu amelitaka Jeshi hilo lisimamie vizuri matumizi ya fedha za miradi zinazotolewa na Serikali ili kuharakisha mchakato wa utekelezaji wa miradi hiyo muhimu.

“Wasimamizi wa miradi inayotekelezwa hakikisheni kuna uwiano kati ya ujenzi wa miradi na thamani halisi ya fedha inayotolewa na Serikali”.

Kwa Upande wake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuridhia kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya kisasa vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini ambavyo vitasaidia kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi

“Katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya sita tunakwenda kushuhudia mapinduzi makubwa ya ununuzi wa vifaa katika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambapo mchakato upo katika hatua za mwisho, tutanunua hadi helikopta za kuzimia moto”

Naye,Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John William Masunga amesema Serikali imeendelea kutatua changamoto za jeshi hilo ikiwemo kununua boti za uokoaji majini, kuwezesha kupatikana kwa mkopo wa masharti nafuu wa Euro milioni 4.9 kutoka Serikali ya Austria kwa ajili ya ununuzi wa magari 12 ya kuzima moto yakiwamo magari mawili yenye ngazi kwa ajili ya majengo marefu.

Ameongeza kuwa Serikali imeliwezesha Jeshi hilo kukamilisha ujenzi wa kituo kikuu cha zimamoto na uokoaji mkoa wa Dar es Salaam katika eneo la Temeke “Serikali pia inatekeleza Mpango wa Serikali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kupata Vitendea kazi vya Dola za Kimarekani milioni 100”

kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule amesema katika kuuenzi Muungano Mkoa wa Dodoma umeadhimisha kwa kukabidhi eneo la ujenzi wa mrana wa mashujaa, michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa masumbwi, uzinduzi wa miradi, dua maalumu na uzinduzi wa majengo ya zimamoto.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.