• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI KUANZA UJENZI WA BARABARA YA NJIA SITA DODOMA

Imetumwa : October 2nd, 2024

Na; Happiness E. Chindiye

     Habari - Dodoma RS

Serikali inatarajia kuanza Ujenzi wa barabara ya njia 6 kutoka katikati ya Jiji la Dodoma itakayounganisha Jiji hili na miundombinu mingine ya usafirishaji ikiwemo uwanja wa ndege wa Kimataifa Msalato, Reli ya SGR na barabara  ya Mzunguko( Ring road) ili kupunguza msongamano katikati ya Jiji.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 02,2024 na Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa ambaye ameeleza juu ya mpango huo Jijini Dodoma, wakati wa ziara yake  ya kikazi ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Barabara ya Mzunguko wa Nje yenye Urefu wa Kilomita zaidi ya 112 ambapo amesisitiza kuwa Serikali inaendelea na Mazungumzo na Benki ya Dunia ili kuwezesha Utekelezaji wake.

Barabara hizo zitajengwa kwa mwelekeo wa mikoa yote minne inayopakana na Dodoma ambayo ni Morogoro,Dar es salaama, Manyara, Arusha, Singida,Mwanza na Iringa na Mbeya.

Kuhusu Mradi huo wa barabara ya Mzunguko “Outer Ring-Road “ Waziri Bashungwa amesisitiza wakandarasi kuendelea kufanya kazi kwa mujibu wa makubaliano ya Mkataba na kwamba Serikali haitoongeza muda wa ukamilishaji wake.

Mradi wa Barabara ya Mzunguko unatekelezwa kwa vipande viwili ambapo Msimamizi kutoka wakala ya Barabara Tanzania TANROADS Mhandisi Herman Laswai na Mshauri Elekezi katika mradi wa kipande cha kwanza wameeleza kusimamia mradi kwa karibu ili uweze kukamilika kwa wakati.

Katika ziara hiyo Mhe. Bashungwa aliambata na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule pamoja viongozi wengine ngazi ya Mkoa na Halmashauri ya Dodoma jiji .

&&&

#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.