• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI KUIMARISHA ULINZI NGAZI YA KATA

Imetumwa : October 4th, 2024


Na: Hellen M. Minja,      

    Habari - DODOMA RS

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ina mkakati wa kuimarisha ulinzi katika ngazi ya Kata kwa kuwaweka Wananchi kuwa karibu na Jeshi hilo na kurahisisha utoaji wa taarifa za viadhiria vya uvunjifu wa amani au matukio ya kihalifu.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 04, 2024 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Hamad Y. Masauni (MB), wakati wa Mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Laikala kilichopo katika kata ya Sagala, halmashauri ya wilaya ya Kongwa ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kikazi katika mkoa wa Dodoma.

Waziri huyo amesema lengo hasa la mkakati huo ni kuimarisha uhusiano mzuri baina ya wananchi kwenye ngazi ya chini ya Serikali na Askari Polisi.

"Serikali inakuja na Mkakati wa kuimarisha ulinzi katika ngazi ya Kata hivyo, imetawanya Askari Kata wengi kwa dhumuni la wananchi kuwa karibu na Askari hawa. Pia Serikali ina mpango wa kujenga vituo vya Polisi Kata katika mwaka huu wa fedha na kukamilisha vituo vyote vilivyojengwa na Wananchi" Mhe. Masauni

Kadhalika, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule, amesema Serikali ya Mkoa inahakikisha inaweka usimamizi madhubuti wa fedha zinazotolewa na Mhe. Rais kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

“Sisi Serikali ya Mkoa wa Dodoma, tutahakikisha tunasimamia kwa umakini mkubwa fedha zote zinazotolewa. Sifa mojawapo ya Kongwa inaongoza katika usimamizi wa miradi. Mwaka 2023, ofisi ya Rais TAMISEMI ilitoa tuzo kwa Halmashauri zilizofanya vizuri kwenye miradi na wilaya ya Kongwa iliongoza kwa kufanya vizuri hivyo fedha nyingi anazozileta zitasimamiwa vizuri” Mhe. Senyamule

Aidha, Mbunge wa Jimbo la Kongwa Mhe. Job Ndugai, amesema hali ya ulinzi na usalama kwenye jimbo lake inaridhisha kwani Polisi Kata wanawajibika kwa nafasi zao.

“Upande wa ulinzi na usalama, tunaye Askari Kata ambaye anajitahidi kuhakikisha watu wake wanakaa kwa usalama kwani 'center' yetu kubwa ya kibiashara haipo mbali na kuna wageni wengi wanaingia, matukio baadhi yanatugusa kwa namna moja au nyingine lakini askari wetu wako imara, wananchi wako salama” Mhe. Ndugai

Katika ziara hiyo, Mhe. Masauni alitembelea na kufungua Mradi uliokamilika wa chumba kimoja cha Maabara ya masomo yote ya sayansi iliyojengwa kwa fedha za ndani za Halmashauri hiyo kwenye shule ya Sekondari Laikala. Maabara hiyo imegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 60.

#dodomatukotayarikujiandikisha

#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.