• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI YAWEKA WAZI UPATIKANAJI WA SOKO LA ZABIBU

Imetumwa : June 18th, 2023

Serikali imeainisha mikakati katika kuhakikisha soko la zabibu linakuwa la uhakikia ndani na nje ya nchi.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde amesema hayo leo Juni 18, 2023 katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Bw. Daniel Chongolo ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake katika Mkoa wa Dodoma ambapo ametembelea Mradi mkubwa wa Umwagiliaji wa Chinangali.

Mavunde amesema mikakati ya Wizara hiyo ni kuhakikisha wanatafuta masoko ya zao la zabibu ikiwa ni pamoja na kuanzisha kiwanda cha kuchakata   zao hilo ili kuwa na uhakika kuhifadhi mchuzi wa  zabibu kwa muda mrefu.

Mkakati mwingine ni pamoja na kutoza kodi kwa mvinyo kutoka nje ya nchi ili kuimarisha soko la ndani na kuendelea kuhamasisha wawekezaji ili katika ujenzi matanki makubwa ya kuhifafhi mchuzi wa zabibu.

"Serikaki imepata mwekezaji mkubwa atakae kuwa anatengeneza juisi na atanunua zabibu kwa wingi. Pia tuko kwenye mazungumzo na TBL waweze kuhifadhi mchuzi wa zabibu kwa muda mrefu" Mavunde amefafanua

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Daniel Chongolo ameiagiza Wizara ya Kilimo na Wizara ya Fedha na Mipango kukutana na kuona fedha zinapatikana na wakandarasi wanalipwa kwa wakati ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya umwagiliaji.

"Dhamira ya Rais Samia na Serikali yake kwenye hii miradi ya uwagiliaji ni kuona tija inapatikana kwa haraka, sasa nendeni mkakae na mje na majibu ndani ya muda ni namna gani mnakwenda kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hii ambayo ina dhamira ya kujenga uhakika wa Kilimo kwa wananchi ili malengo ya Rais na Serikali anayouongoza yafikiwe kwa muda uliokusudiwa na si vinginevyo."

"Hatutakuwa na maana kama tutakuwa na miradi yenye majina mazuri yenye dhamira njema na isilete matokeo kwa wakati."

Aidha, Changolo pia amekitaka Chama cha ushirika wa Kilimo cha zabibu, kuanzisha Mfuko ambao utatumika kufanya matengenezo kwenye miundombinu ya umwangiliaji katika mashamba ya ushirika huo.

Kuhusu soko la zabibu, Chongolo amewataka kutofikiria ununuzi wa zabibu kutoka nje bali kuwa na uzalishaji wa bidhaa ya mwisho wa zao la zabibu ndani ya nchi.



Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.