• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SHIRIKA LA “SAVE THE CHILDREN LAIKABIDHI SERIKALI YA MKOA WA DODOMA MRADI WA CONNECT

Imetumwa : November 22nd, 2024

Na;Sofia Remmi

Habari - Dodoma Rs

Mkuu  wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule ametaja faida za kutumia uzazi wa mpango kuwa ni pamoja na kusaidia kupunguza mimba za utotoni, kupunguza hatari ya vifo vya mama  na mtoto wakati wa kujifungua, na kutoa nafasi kwa vijana kufikia ndoto zao.

Mhe. Senyamule ameyasema hayo Novemba 22, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Mesuma Jijini Dodoma  wakati wa hafla ya  kufunga mradi wa Connect uliokuwa chini ya Shirika la 'Save the Children' ukiwa na lengo la kuongeza mwitikio chanya wa utumiaji wa huduma za afya ya uzazi,na uzazi wa mpango kwa akina mama vijana  wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24.

"Takwimu za Kitaifa za  kati ya mwaka 2015/2016 zinaonyesha  27%  ya wasichana wa umri kati ya miaka 15 hadi 19 wanakuwa tayari wamepata ujauzito.Kwa mkoa wa Dodoma ilikuwa ni asilimia 39.

 Jitihada mbalimbali zilizofanywa na Wadau kwa kushirikiana na Serikali zimesaidia kupunguza idadi ya wasichana wanaopata ujauzito hadi kufikia asilimia 22.7 Kitaifa na kwa mkoa wa Dodoma imefikia asilimia 21.2 na huu ni utafiti uliofanyika mwaka 2022,” amesema Mhe Senyamule

Aidha Mhe .Senyamule amempongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi ya kuwasaidia akina mama vijana walioingia katika jukumu la uzazi wakiwa na umri mdogo kupata haki ya kuendelea na masomo baada ya kujifungua.

Kwa upande wake Meneja Mradi wa Connect Bi.Lilian Kapinga amesema mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka  2019 katika halmashauri za Bahi na Kongwa na unatarajia; kukamilika ifikapo Disemba mwaka huu,  ambapo mradi huo ulikuwa unatekelezwa na Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na shirika la 'Save the Chirdren' na TAHEA.

“Katika utafiti tuliofanya tulibaini kuna vikwazo vinne vya kuzuia wanawake kutumia uzazi wa mpango ambavyo ni  suala la maamuzi, dhana potofu, vijana wengi wanasahaulika na uduni wa elimu ya uzazi wa mpango. Mradi huu ulilenga kuboresha na kutatua changamoto hizo kwa  makundi hayo,”amesema Kapinga

Awali Meneja wa Save the Chirdren Mkoa  Bi.Mariam Mwita ameweka bayana lengo la hafla hiyo  kuwa ni kufanya hitimisho la mradi pamoja na kukabidhi rasmi vitendea kazi na rasilimali za mradi kwa serikali ya Mkoa  kuhakikisha uendelevu na kusaidia juhudi za upanuzi wa mradi siku za mbeleni na  kuhakikisha vijiji vyote vya Mkoa wa Dodoma vinafikiwa.


#kurayakosautiyako

#ujanjanikupigakura

#dodomatukotayarikupigakura

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.