• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TAKUKURU YAAGIZWA KUCHUNGUZA MRADI WA SHULE

Imetumwa : November 16th, 2022


“Wapo walioomba kuongezewa Milioni 90 au 70 lakini waliweza kuchimba visima virefu vya maji, wakachonga na barabara za kuweza kufika kwenye shule zao, lakini kwa ujenzi tu wa madarasa? Angalau ningesikia uongezwe Milioni 20 au 30 ingekua tija lakini kwa hii, hapana. Naagiza TAKUKURU waje wafanye uchunguzi kwenye ujenzi wa shule ya Iwondo labda kuna kitu hakipo sawa.” RC Senyamule

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipofanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa shule ya sekondari ya mfano ya Iwondo pamoja na madarasa yanayojengwa kwa fedha za Serikali katika shule mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ambayo ni miongoni mwa Halmashauri zilizo nyuma ya wakati kwenye ujenzi.

Shule ya sekondari Iwondo ni moja kati ya shule 11 za Mkoa wa Dodoma zilizopewa fedha za Serikali za mradi wa SEQUIP wenye thamani ya Shilingi Milioni 600 lakini baada ya ukaguzi huo, imeonekana haina ubora unaokidhi kiasi hicho cha fedha

“Ukiona yale madarasa ya shule ya mfano ambayo imepewa Milioni 470 awamu ya kwanza na awamu ya pili ilipokea Milioni 130 na bado ipo nyuma. Shule nyingine zilizo kwenye mradi huo tayari zimeshasajiliwa kwa ajili ya kuanza kidato cha kwanza mwakani, sasa hii ambayo inaonekana bado safari yake ni ndefu, tumeweka maswali mengi” RC Senyamule.

Mbali na kutembelea mradi wa shule hiyo ya Iwondo, pia Mhe. Senyamule ametembelea ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari za Chipogoro iliyopokea shilingi Milioni 60 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu ambapo mradi bado upo nyuma ya wakati. Kwenye shule ya sekondari Massa iliyopokea Milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa darasa moja nayo bado haijafikia kiwango cha kukamilisha mradi kwa wakati.

Shule ya mwisho kuitembelea katika ziara hiyo ni sekondari ya Ipera ambayo imepokea shilingi Milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili, nayo bado haijafikia kiwango cha kukamilisha ujenzi ambacho kimepangwa na Mkoa kukamilika tarehe 5 Desemba mwaka huu kwa ajili ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza 2023.

Maagizo yametolewa na Mkuu wa Mkoa kwa shule zote hizo ambazo hazijakamilisha ujenzi kuwa ingawa kuna mapungufu yaliyojitokeza wakati wa ujenzi lakini Mkurugenzi wa Halmashauri afanye kadri anavyoweza kuhakikisha shule hizo zinakamilisha ujenzi kwa wakati na kwa kiwango kinachokubalika kwani aliahidi mwenyewe kumalizika kwa miradi yote kwa wakati kwenye makubaliano aliyoweka na Mkoa.

Akielezea namna ya kukabiliana na changamoto hizo zinazokwamisha miradi kukamilika kwa wakati, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpwapwa Bi. Mwanahamis Ally, amesema;

“Kitu kikubwa kama ambavyo imetokea kwenye maeneo yetu yote ya ujenzi, ni changamoto ya upatikanaji wa vifaa vya ujenzi lakini Pamoja na hilo, tumefanya juhudi za upatikanaji wa vifaa hivyo an ampaka sasa vipo tayari lakini tatizo tulilolibaini ni upungufu wa mafundi, juhudi kubwa niliyoifanya ni kupita site kuhakikisha mafundi wanaongezwa. Kwa mikakati hii, tunahakika kufikia tarehe 5 kila kitu kitakua tayari na tutakabidi miradi” Bi Mwanahamisi

Kadhalika, Mkandarasi kutoka Mkoani ambaye ameambatana na Mkuu wa Mkoa kwenye ziara hiyo, Mhandisi. Victor Kajuma, ametoa tathmini yake juu ya miradi ya shule hizo kwenye Halmashauri hiyo na kumshauri Mkurugenzi kuongeza Mkandarasi kwani itasaidia kwenye usimamizi ambapo kwa sasa ujenzi wote unasimamiwa na mkandarasi mmoja ambaye inakuwa changamoto kwake kusimamia miradi kwa ufasaha.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, aliitisha kikao na wakurugenzi wote wa Halmashauri zote nane za mkoa wa Dodoma mwezi Septemba kwa ajili ya kuweka mikakati na makubaliano ya kukamilisha miradi ya ujenzi wa shule za mfano 11 za SEQUIP pamoja na madarasa 339 kwa Mkoa wa Dodoma, ambayo imetolewa fedha na Serikali na makubaliano yalikua kila Halmashauri ihakikishe inakamilisha miradi yote na kuikabidhi ifikapo tarehe 5 Desemba tofauti na muda wa Wizara ya Elimu ambao ni tarehe 15 Desemba.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.