• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

“TANZANIA NI NCHI PEKEE AFRIKA KUDUMISHA AMANI MIAKA 61 YA MUUNGANO” - WASIRA

Imetumwa : April 23rd, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Imeelezwa kuwa miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa nchi ya Tanzania mnamo Aprili 26, 1964, umeifanya Tanzania kuwa nchi pekee Barani Afrika kuweza kudumu na Amani licha ya uwepo wa Baadhi ya nchi katika Bara hili zinazotawaliwa na uvunjifu wa Amani ikiwemo uwepo wa Mapinduzi ya kisiasa kila uchao.

Hayo yamebainishwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ndugu Steven Wasira wakati wa ziara yake katika Mkoa wa Dodoma iliyoanzia kwenye Wilaya za Chamwino na Bahi Aprili 23, 2025 inayolenga kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano.

“Kwa miaka 60, nchi hii inayoitwa Tanzania imekua nchi ya pekee katika Afrika ambayo imedumu na Amani kwa miaka 60. Tunawashukuru viongozi wetu wa Majeshi ya Ulinzi kwani wameonesha uzoefu wa hali ya juu sana kwani nchi za Afrika zimekua zikipinduliwa kila mwaka. Sisi tangu mwanzo tumeonesha uwezo wa kisiasa wa kujitegemea na kujitawala” Amesema Ndugu Wasira.

Akizungumza na hadhara iliyojitokeza kumlaki Makamu Mwenyekiti huyo katika viwanja vya Bahi Sokoni, Wilaya ya Bahi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma ndugu Alhaji Adam Kimbisa amesema miradi mingi iliyotekelezwa na Mhe. Rais Samia katika Wilaya hiyo ni utekelezaji wa ilani ya Chama hicho Tawala hivyo, watu wa Bahi wanatakiwa kujivunia hilo.

Kadhalika, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema; “Sisi tutoe shukrani za kipekee kwa Mhe. Dkt Samia kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya katika Mkoa wetu wa Dodoma na amefanya utekelezaji wa Ilani ya chama kuwa rahisi kwetu.

Dodoma tunayo miradi ya aina tatu, miradi ya kimkakati, miradi kwa ajili tu ya huduma wananchi wa Dodoma na miradi kwa ajili ya kuhudumia wananchi wote wanaokuja Makao Makuu ya Nchi. Miradi hiyo yote katika historia ya miaka minne ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia kuanzia mwaka 2021ina gharimu zaidi ya Trilioni 10 ya fedha za Kitanzania.”

Aidha, katika ziara hiyo, ndugu Wasira alitembelea na kuweka jiwe la Msingi kwenye mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Amali katika Kata ya Nzali, Wilaya ya Chamwino ambayo inagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.6 pia katika Wilaya ya Bahi, ametembelea Hospitali ya Wilaya hiyo ambayo imekamilika na inatoa huduma za Kitabibu kwa wananchi.

Ziara ya siku nne ya Ndugu Wasira katika Mkoa wa Dodoma iliyoanza Aprili 23 na kutarajiwa kutamatika Aprili 26, itatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya kimkakati na maendeleo inayotekelezwa Mkoani hapa sanjari na kuzungumza na wananchi juu ya umuhimu wa kulinda Muungano kwenye Wilaya zote saba (7) za Mkoa huu.


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

#karibumwengewauhuru2025mkoawadodoma

#miaka61yamuunganowatanzania2025

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.