• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

THAMANI YA UWEKEZAJI MFUKO WA PSSSF KUFIKIA SH.TRILIONI 7.98-MAJALIWA

Imetumwa : August 12th, 2023


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kiwango cha thamani ya uwekezaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) imeongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 7.98 kwa mwaka 2022/2023 kutoka shilingi trilioni 7.5 kwa hesabu za mwaka wa fedha ulioishia Juni, 2022.

Amesema hayo leo (Jumamosi, Agosti 12, 2023) wakati wa maadhimisho ya miaka mitano ya mfuko huo na uzinduzi wa huduma za wanachama kidijitali, kwenye ukumbi wa PSSSF jijini Dodoma.

“Thamani hii ipo katika soko la hisa ambalo ni kichocheo kikubwa katika ukuaji wa mitaji nchini ambapo mfuko huo ni muwekezaji mkubwa wa ndani mwenye hisa katika makampuni makubwa kama CRDB Bank Plc, NMB Bank Plc, Tanzania Breweries Limited, na Vodacom Tanzania Plc. ”

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ameitaka Mifuko ya Hifadhi ya jamii kufanya uwekezaji wenye tija kwa wanachama na jamii inayolingana na thamani ya fedha za wanachama “Fanyeni utafiti wa kina kubaini masoko ili uwekezaji unaofanywa usilete hasara kwa mifuko. ”

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameiagiza mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii kuendelea kulipa mafao kwa wakati ili kuleta utulivu kwa wanachama. “Wazee wastaafu wasisumbuliwe, kumbukeni kuwa sisi sote ni wastaafu watarajiwa. ”

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ameziagiza taasisi za Serikali kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati uzinduzi wa mkongo wa mawasiliano wa 2Afrika na matumizi ya teknolojia ya 5G la kutaka taasisi zote za Serikali ziwe zinasomana ili kurahisisha na kuboresha utoaji wa huduma kwa Watanzania.

Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof Joyce Ndalichako amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa maono na dhamira ya dhati ya kuimarisha sekta ya hifadhi ya jamii “lengo la Rais Samia ni kuona inafanya kazi kwa tija, ufanisi na kutoa huduma bora. *

"Tunampongeza pia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia kwa uthubutu wa kutoa fedha kwa mfumo wa hati fungani shilingi trilioni 2.17 za kulipa deni ambalo lilimedumu kwa muda mrefu, mfumo huu umewezesha PSSSF kulipa wastaafu kwa wakati.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amesema PSSSF ni kimbilio la wananachi bila kujali wanatoka mahali gani ni kiashiria kuwa sasa wanajali na kuthamini wadau wao katika maeneo tofauti tofauti na wameendelea kuwekeza katika maeneo mengi.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.