• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

"Tukatende Haki, Sitarajii Kuona Makosa ya Taariza Za Sensa Yatokee Mkoa wa Dodoma"- Rc. Rosemamry Senyamule

Imetumwa : August 6th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe .Rosemary Sitaki Senyamulke ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kutembelea madarasa ya makarani wa sensa yanaondelea jijini Dodoma.

Mhe.Senyamule amaewataka wananchi na makarani wote wa sensa,mkoa wa Dodoma,kumshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu kubwa tatu,  inabidi wamshukuru sana mosi, kwa kuridhia na kutoa fedha za sensa, pili kwa utashi wa kuamua sensa iwe ya watu na makazi.Tatu, kwa kutumia vijana ambao wamesoma lakini hawana ajira kushiriki katika zoezi la sensa, kwani angeweza kuelekeza watumishi tu ndio watumike kwenye zoezi hili,lakini hapa mpo mchanganyiko wa watumishi wa Umma na wasio watumishi huku wengi wenu mkiwa vijana.Hii inaonyesha wazi dhamira njema ya Mhe. Rais kwa vijana wa kitanzania. Hivyo nendeni mkaonyeshe kuwa mna uwezo mkubwa ila tu nafasi za ajira ni chache.

Sisi kama Mkoa tunatamani tuwe wa kwanza kuliko mikoa mingine.Tunajua kuwa mnaaminiwa lakini mkaonyeshe kwa matendo.Tumekuja na Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa (KUU) ili mjue umuhimu wa zoezi hili.Kufanya kosa Katika Sensa ni kuhujumu Sensa.Kama RPC ana uwezo wa kukamata mwizi asiyemjua  hivyo endapo yeyote kati yenu kwa maksudi atakiuka taratibu, kanuni na sheria za sensa,basi mjue ya kuwa sheria itafuata mkondo wake. Ili kuepuka yote hayo mkafanye kazi kwa uadilifu.Tukatende haki, Sitarajii kuona makosa ya sensa yatokee Mkoa wa Dodoma.Tutatoa namba kwa wananchi Ili endapo kuna tatizo lolote na hajahesabiwa  basi aweze kutoa taarifa.Sisi hatutakuwepo ila wananchi watatutaarifu. Aidha niwatakie mafunzo mema na utayari wa kulitumikia Taifa kwani Mhe.Rais amewatakia mema nanyi mnatakiwa kumtakia mema.

Akizungumza dhumuni la ziara hiyo, katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga amesema tumekuja kuwaangalia mnaendeleaje na mafunzo na nikiwa mtendaji mkuu ninaye shughulika na  wsatumioshi ninapenda kuwakumbusha mambo machache, kwani hapa mlipo baadhi yenu ni watumishi  wa Umma na wengine si watumishi wa Umma. Hivyo hapa tunaongea na watumishi wa kudumu na wasio wa kudumu. Mnapoenda kufanya zoezi la sensa fanyeni Kazi kwa uadilifu.Simama wewe kama wewe.Hatutegemei dodoso lolote lilete sintofahamu au kuharibika kwa takwimu. Mapokezi na wimbo wenu unaonyesha wazi  kwamba mnajitambua. “Mkajifunze kwa bidii na siku mbili mtakazopewa kabla ya kuanza zoezi lenyewe basi hakikisheni kwamba unaijua kaya yako vyema. Nendeni mkawatumikiie watanzania kwa moyo wote.Usiruke kaya hata moja.Uadilifu na uvumilivu ni vya muhimu sana kwani Vijana mnaharaka, hatutegemei – subcontract,nenda kakamilishe kila kitu wewe mwenyewe.Tengeneza mahusiano mazuri na wenye kaya.Uadilifu katika nyanja zote.Mnapoingia kwenye kaya mkatumie lugha nzuri.Sitegemei kuona karani wa sense toka Mkoa wa Dodoma ambaye hatakuwa na mahusiano mazuri.Mnapaswa kutunza Siri za watu.Hampaswii kushangaa shangaa bila sababu,Lugha zetu ziwe nzuri.Kajifunze Community yako inahitajinini.Tutaendelea kuwa fuatilia.Tuonyeshe uzalendo wetu kwa vitendo.Tumshirikishe Mungu Ili zoezi likafanikiwe.Tukawe Taswira Katika Mkoa wa Dodoma”.Amesisitiza Dkt. Mganga.

Nae Mkuu wa Wilalya ya Dodoma Jiji Mhe. Jabbir Shekimweli, ameeleza kuwa jumla ya watu walioomba nafasi za ukarani wa sense ilikuwa 13000, baada ya Mchujo wa kwanza wakabaki 11,000 wakati hitaji halisi ni makarani 2068 na hivyo watu walioachwa/ kukosa nafasi ni takribani 9000.Hivyo kwa nyie mliopata fursa hii adhimu ni vyema mkuitumia vyema fursa hii.Aidha  Mhe. Shekimweli ameeleza  na kutoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa  kuendeleza ujenzi katika mji wa serikali ambapo ujenzi wa ofisi /majengo 20 ya ghorofa yenye thamani ya Tsh.300.0bln,unaendelea, reli ya SGR ambapo ikikamilika Dodoma / Dar itakuwa masaa matatu tu, kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Msalatio , Barabara ya Pete /ring road, kiwanda cha mbolea amacho kitazalisha ajira ya watu 10,000.hivyo mkiwa makarani wa sense kutoka mkoa wa Dodoma mnapaswa kuonyesha shukrani zenu za dhati kwa mhe. Rais kwa kufanya kazi ya ukarani kwa uadilifu mkubwa,ili kwa wale ambao bado si watumishi baadae mkapate kipaumbele enda Serikali itakuwa na kazi nyingine yeyote.MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.