• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TUME YA KUDHIBITI UKIMWI TANZANIA ( TACAIDS) YATEMBELEA OFISI YA RC DODOMA

Imetumwa : September 13th, 2022

Uongozi wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TANZANIA)- TACAIDS hivi karibuni umetembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma kwa lengo la kujitambulisha na kutoa mrejesho wa shughuli  mbalimbali zinazofanywa na  Tume hiyo Mkoani Dodoma.

Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Tume Ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dkt.Leonard Maboko, amesema TACAIDS ina Makamishna kumi na moja (11) ambao ndio Bodi ya Utendaji. Pamoja na makamisha hao kuna sekretarieti ya Tume.Aidha, Makamishna wa Tume wanawakilisha kila sekta inayogusa jamii ikiwa ni pamoja na wawakilishi kutoka mashirika ya Dini,Sekta Binafsi, Vyuo Vikuu , vijana na kadhlika . Dkt. Heviga Swai ndiye mwenyekiti wa TACAIDS.

Baada ya Utambulisho huo, Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule ameukaribisha ujumbe huo na kuwashukuru kwa kuchagua kutembelea Dodoma.”Hongera sana kuchagua Dodoma. Hongera sana kwa kazi mnayofanya, hasa kwa kupambaa kufikia zile sifuri 3 ifikapo 2030, sifuri ya kwanza ikilenga kuzuia maambukizi mapya, sifuri ya pili kupunguza vifo na sifuri ya tatu kukomesha unyanyapaa wa wagonjwa wenye ukwimwi.Pongezi kubwa kwani kwa sasa maambukizi, vifo na unyanyapaa umepungua kiasi kikubwa kiasi cha kwamba hadi watu wanasahau kupima, hali ambayo  ni hatari kwa jamii. Mkoani Dodoma masuala ya UKIMWI yanabidi yaongezewe nguvu kwani tuna vijana wengi sana kutoka na ongezeko la vyuo vikuu,pia wakati huu kuna vijana wengi sana ambao wazazi wao walikufa na kuwaacha na maambukizi hivyo ni vyema hasa vijana wakaelimishwa. Aidha mkoa wa Dodoma ni Mkoa wa Sita (6) Tanzania kwa kuwa na watoto wanaopata mimba wakiwa bado shuleni.Hivyo tunawakaribisha Dodoma ili  muweke program maalum kwa masuala ya UKIMWI.Siku hii moja mtakayotembea Dodoma tunategemea mje na ushauri.

Nae katibu tawala mkoa wa Dodoma  Dkt. Fatuma Mganga  ametoa shukrani kwa uongozi wa TACAIDS na kusifia  mradi wa TIMIZA MALENGO, mradi ambao umekuwa na manufaa na mafanikio makubwa sana mkoani Dodoma.

Akitoa taarifa Kuhusu hali ya UKIMWI mkoani Dodoma Mratibu wa kudhibiti Ukimwi Mkoa pamoja na matibabu Dkt. Abdul Ahmed amesema kuwa kulingana na taarifa ya 2016/2017 hali ya ushamiri na maambukizi ya UKIMWI mkoani Dodoma ni 5%,  ambapo watu 52,242 wanahisiwa kuishi na VVU na wagonjwa wengi wanapatikana  maeneo ya Dodoma jiji na halmashauri ya wilaya ya Kongwa. Katika vituo 356 vya  kupimia VVU, Wanawake wajawazito  103,200 walipwa VVU kati yao wanawake 1035 ndio waligundulika kuwa na VVU ambao ni   sawa na 1.26%. Wanawake hawa  walipewa RV, baada ya kujifungua na baada ya vipimo ni watoto 4 waliokutwa na VVU. Mkoa umeanzisha zoezi la kuhakikisha watu wanabaki kwenye matumizi ya dawa za kufubaza UKIMWI japo wengi wamekuwa wakitoroka au kutoenda kufuatilia dawa hali ambayo  ni hatarishi kwa maisha yao na kuletelea kutoka mfumo.

Tayari tuna watumishi 3,750 wanaofanya kazi ya kuhakikisha watu wanarudi kwenye mfumo . Baada ya zoezi hili kuanza  tayari watu 1635 walikuwa tayari kurudi kwenye mfumo. “Mkoa wa Dodoma ni kati ya mikoa 5 ambayo ipo katika mradi wa TIMIZA MALENGO.Mradi huu hutoa ruzuku kwa wasichana ambao bado wapo shule ambapo wana mahitaji mbalimbali na wazazi/ walezi wao hawana uwezo wa kuwawezesha. Mradi huu huwawezesha wasichana hao kupata kiasi cha Tsh.25, 000/- kwa mwezi na fedha hizo hutoka kila baada ya miezi 2 kupitia TASAF, lengo kusaidia watoto wapate mahitaji yao. Kiasi cha Tsh 1.546 bln zimetolewa kwa zoezi hilo na tayari Tsh 1.130 bln zimepelekwa kwa wanafunzi kupitia TASAF. Aidha Msaada kuandika andiko la kupata Tsh.1.8bln kwa wanafunzi walio nje ya mfumo umetolewa na wasichana balehe 3,287 wamefundishwa. Vilevle mradi wa TIMIZA MALENGO umetoa msaada na Kugawa Taulo  za kike kwa wanafunzi wa kike ili waendelee na masomo”.Amesema Dkt. Ahmed.

Ujumbe wa TACAIDS upo Mkoani Dodoma kwa ziara ya siku moja.MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.