• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

“TUNAJIVUNIA KUISHI WALICHOANZISHA WENGINE ILI TUPATE MATOKEO “ - RAS MMUYA

Imetumwa : November 18th, 2024

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya, ameshiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la JK Square lililopo ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakati wa maadhimisho ya kumbukizi za siku za kuzaliwa kwa waliozaliwa mwezi Novemba, tarehe 18,Novemba, 2024.

Maadhimisho hayo ambayo huenda sambamba na kampeni ya ‘mti wangu, birthday yangu’  inayohamasisha watu kupanda miti ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya siku zao za kuzaliwa lakini pia kuifanya  Dodoma kuwa ya kijani.

“Tumechagua program hii bila kujali alianzisha nani haya maneno, sisi tunayaishi kwa vitendo. Tupande, miti kwenye matukio yetu ya birthday, lengo letu ni kuleta matokeo ya mawazo mazuri yote wanayoanzisha watu duniani. Tunajivunia kuishi walichoanzisha watu ili tupate matokeo dunia hii iwe ‘green’ Amesema RAS Mmuya.

Hata hivyo, mwakilishi wa uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma Profesa Albino Tenge amesema eneo lililopandwa miti lina historia maalumu na limewekwa rasmi kama mahali pa kupumzika kwa kupata kivuli kwani watu wengi wakifika Dodoma, hupenda kutembelea UDOM na sasa watakua na mahali maalumu pa kupumzikia.

Naye Msimamizi wa eneo hilo ikiwa ni pamoja na zoezi zima la upandaji miti na kupendezesha Mhandisi David Chitemo amesema;

“Tulianza kwa kusafisha eneo hili lenye ukubwa wa ekari 7 lakini eneo lote lina ekari 10, awamu ya kwanza ya uzinduzi tulipanda miti 780 iliyohusisha miti ya matunda na miti mingine ya kawaida. Tumeongeza mashimo 492 ambayo ndio imepandwa leo. Miti iliyopandwa mwezi wa 10 ni miti 7 tu ndiyo iliyokufa lakini tumeweka mingine mipya”. Mhandisi Chitemo.

Kampeni hii iliyoasisiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya, ni endelevu kwa kila tarehe 18 ya mwezi ambapo wazaliwa wa mwezi husika watafanya kumbukizi zao kwa kupanda miti kwa lengo la kutengeneza maeneo ya kupumzikia katika Jiji la Dodoma.


#kurayakosautiyako              

#ujanjanikupigakura              

#dodomatukotayarikupigakura

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.