• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

"Tusing'ang'anie Kuwa na Idadi Kubwa ya Mifugo, Tuwe na Mifugo Inayoendana na Malisho Yetu"-Mhe. Mashimba Ndaki

Imetumwa : August 5th, 2022

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki, ameyasema hayo leo wakati wa sherehe za ufunguzi wa Nanenane kanda ya kati ambayo inahusisha mikoa ya Dodoma na Singida.Mhe.Mashimba amewashukuru wale wote walioshirki maandalizi ya 88 kwani taarifa za maonesho ya Nanenane zilichelewa hata hivyo kamati ya maandalizi imefanya kazi kubwa sana, pongezi kwa kamati ya uratibu kanda ya kati.

Aidha Mhe. Ndaki amempongeza mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule kwa kuaminiwa na Mhe. Rais na hatimae kuhamishiwa makao Makuu ya nchi. “Dodoma ni makao makuu ya nchi, hivyo kwa kuhamishiwa Dodoma inaonyesha kwamba Mhe. Rais ana imani na wewe  kwamba utamsaidia “. Amesema Mhe. Ndaki.

"Maonesho ya Nanenane  yanalenga katika kujitangaza lakini pia na kutoa elimu. Mwaka huu maonesho ya nanenane  mkoa wa Dodoma ni maonesho ya 14 na paredi ya 11. Paredi hii ya  imehusiha watu wachache hivyo ni matumaini yangu kuwa Paredi ya mwaka kesho (2023) itajumuisha  watu wengi zaidi. Hongereni sana  kwa ubunifu huu mzuri. Taarifa yetu ya uchumi , inaonyesha ukuaji wa kilimo umepungua kufikia 3.39% (2021)  toka 4.99%(2020)  ikionyesha kwamba umepungua kwa 1%. Sababu za upungufu huo ni pamoja na ukame/ ukosefu wa mvua pamoja na Uviko-19. Hata hivyo Serikali imepanga tutoke kwenye kilimo cha kujikimu na kuhamia katika  kilimo cha kibiashara. Kilimo chetu kinakabiliwa na Changamoto ya tabia nchi, kwa kuliona hilo serikali imeongeza bajeti za kilimo, mwaka huu zimetengewa fedha za kutosha na hivyo kusaidia kukabiliana na Changamoto hizo.

Mhe. Ndaki ameagiza taasisi zinazofanya tafiti za kilimo, Zifanye tafiti ambazo zitasaidia  wananchi kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tumegusa maisha ya wananchi. Bei ya bidhaa Kwa wananchi zipo juu sana. Ili bidhaa hizo ziweze kuwafikia watanzania basi ni bora bei ziendane na kipato cha wananchi.Pamoja na ubora wa bidhaa zetu ni lazima tuangalie jinsi ambavyo tunapakia/tunafunga bidhaa zetu. Kwani tunatakiwa kushindanisha ubora ambao ni pamoja na jinsi bidhaa ilivyofungwa. Aidha Mhe. Ndaki amewaasa wananchi kutong’angania kuwa na idadi kubwa ya Mifugo, badala yake wafuge mifugo inayoendana na malisho yao. Mhe. Ndaki amewakumbusha wananchi Wote wajiandae kuhesabiwa na kuepukana na  wapotoshaji.

Akizungumza Mkuu wa Mkoa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amemshukuru Rais wa Jamhuri wa Mungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini ya mara ya pili. Mkoa wa Dodoma una takribani watu 2.7 milioni, 72% ya watu hao  hutegemea Kilimo & Mifugo na UVuvi.

Aidha Mhe. Senyamule ameeleza kuwa Mkoa una idadi ya mifugo 5.64 mln ambapo kati yao ng’ombe wa kienyeji ni 1.53mln na  242,000 ni ngombe wa kisasa. Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa Mkoa wa Dodoma una eneo la ufugaji wa samaki, tunayo teknolojia ambayo itatupelekea kufuga samaki kwa njia ya kisasa. Rai yangu sisi hapa Dodoma tutajitahidi sana kuona kwamba tunafuga na kujitosheleza kwa samaki. Kwa upande wa kilimo mwaka huu tumeweza kuvuna 55% kwa sababu tulitegemea mvua.  Dodoma imeanishwa kama mkoa mmoja wapo kati ya mikoa mitano ambayo inafaa wa kulima alizeti.Hivyo kazi yetu kubwa tuliyo nayo Dodoma, ni kuhakikisha kuwa tunafanya kazi kwa bidii na kuifanya Dodoma, Dodoma ya Samia.

 "Nitumie fursa hii kuwakumbusha Mambo matatu, kwanza Mkoa wa Dodoma ni mkoa mmojawapo wenye ukubwa wa vyuo vikuu.Hivyo tunataka  tuone matokeo ya vyuo vikuu Dodoma kwa wananchi wa Dodoma. Jambo la pili Machinjio yamelegalega kwa hiyo itabidi tukutane na tuongee namna tunavyoweza kuyaboresha.Tatu, 16/8/2022, Wananchi wote wajitokeze kwa wingi kwenye maeneo yote ambayo Mwenge utapita.Pia kutakuwa na Sensa ya watu na Makazi 23/8/2022 ".amesema Mhe. Senyamule.

Aidha Mkuu wa Mkoa amemwelea Mhe. Waziri,kuhusu uwanja wa nanenane Nzuguni kuwa  ni uwanja mkubwa sana hivyo nitaomba tukutane ili tuone namna bora ya kuboresha huu uwanja na ili  uonekane kuwa ni wa makao makuu.

Kaimu Katibu Mkuu, Dkt.Charles Mhina ambaye amemwakilisha Bw.Tickson Nzunda Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi – Sekta ya Mifugo ameeleza kuwa Wizara inaendelea kuboresha na kuzalisha mbegu kupitia vituo vyao mbalimbali  na inajipanga kutoka kwenye ufugaji usio na tija hadi ufugaji wenye tija. Aidha ameahidi kuwa watandelea kuimalisha uzalishaji kwa kuwapatia wafugaji mbegu za malisho, ili wafugaji nao waweze   kuzalisha kwa kutumia tija.

Nae  Katibu Mkuu sekta ya Uvuvi. Rashid Tamatama . Ametoa shukrani kwa kamati ya maandalizi na wana Dodoma kwa maandalizi mazuri. Kwani maonesho haya yanawapa fursa wananchi kujua sekta ya mifugo na uvuvi. Mwaka 2021 sekta ya uvuvi imeongeza Vizimba 731 ambavyo vimelenga wafugaji wadogowadogo na katika ziwa Victoria.Serikali imedhamiria kupunguza mazao ya uvuvi na kuongeza thamani."Tumepanga kuongeza uzalishaji kimkakati kwa ujenzi wa bandali ya uvuvi Kilwa. Tumeboresha huduma za ugani. Hivyo endapo unataka kuanza ufugaji wa Samaki fika ofisini na wataalam watakuelimisha. Nawasihi wananchi wa Dodoma na Singida kuhudhuria kwa wingi ili kuweza kujifunza masuala ya mifugo na uvuvi’’.Amesema Tamatama.

Akizungumzia paredi ya Wanyama, Jeremia Temu kiongozi wa paredi ya mifugo,ameeleza lengo la paredi hiyo ni kutoa elimu kwa wafugaji kuwa na  ufugaji wenye tija unawezekana na kuonyesha fursa za kibiashara kwamba wanaweza fanya ufugaji bora.Paredi hii itaonyesha kwamba ufugaji bora unawezekana na Ufugaji bora  huanza na mbegu bora zilizothibitishwa. Paredi hiyo ilianza kwa kuonyesha ngombe wa maziwa, ngombe wa nyama na hatimae mbuzi. Ngombe mbalimbali walipita na kuonyesha manufaa yake. Ngombe waliopita ni pamoja na Ng’ombe wa maziwa Mama Tony ambaye anzalisha lita 22 za maziwa kwa siku, Gwasi lita 33 kwa siku,Morning light Lita 30 kwa siku, Mkombozi  lita 28 kwa siku, Mathayo lita 16 kwa siku. Aidha pamoja na ng’ombe wa maziwa Ngombe wa Nyama nao walipitishwa kwenye paredi hilo ambapo ng’ombe  Mahinyila ana 579kg,Masanja 590kgs na Kikwete700kgs.

Akimalizia Mratibu wa Nanenane Bi. Aziza Mumba ameeleza kuwa haya ni maoenesho ya 14 na paredi ya 11, ambapo kutakuwa na  mashindano ya wanyama kwa  wafugaji wakubwa na wafugaji wadogo.Kutakuwa na  Makundi manne ya ushindani.Lengo letu la hapo baadae ni kuufanya uwanja wa Nanenane Nzuguni kuwa uwanja wa viwango vya kimataifa.

MWISHO.

 

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.