• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

UBORESHAJI MIUNDOMBINU YA ELIMU CHACHU YA KUINUA UFAULU DODOMA

Imetumwa : March 15th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS


Mapinduzi ya kipekee yamefanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wake Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, kuimarisha elimu kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu kwa kuweka miundombinu ya kisasa inayosaidia walimu kufanya kazi na wanafunzi kusoma katika mazingira bora na salama.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, ameyasema hayo Machi 15, 2025 wakati wa sherehe ya kuwapongeza Walimu wa Wilaya ya Kongwa kwa kuongeza ufaulu katika mitihani ya Taifa shughuli iliyofanyika katika eneo Godauni, stendi ya mabasi.


“Serikali ya awamu ya sita ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya mapinduzi ya kipekee, imeimarisha elimu kuanzia ngazi ya chini kabisa mpaka ya juu kabisa kwa kuweka miundombinu ambapo kwa Mkoa wa Dodoma ni takribani 24% ya miundombinu iliyojengwa tangu uhuru wa nchi yetu, hili ni jambo la kipekee.


“Leo hii tunashuhudia Kongwa ilivyochangia kwa kiasi kikubwa Mkoa wa Dodoma kuongeza ufaulu kwa 5.3% ndani ya mwaka mmoja kwenye matokeo ya Darasa la saba. Kazi hii mnayoiona ni taa nyekundu kwa watu wa Bahi, ni rahisi sana kuwa namba moja lakini ni kazi kubwa kubaki namba moja”. Ameongeza Mhe. Senyamule.


Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mayeka S. Mayeka amesema Mhe. Rais ameboresha miundombinu ya elimu ambayo inatakiwa kuendana na matokeo mazuri hivyo hili lililofanywa na Wilaya yake, linaleta tafsiri ya uwekezaji bora kwenye elimu.


Hata hivyo, Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Mwl. Vicent Kayombo ambaye pia amemuwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Bw. Kaspar Mmuya amesema Halmashauri ya Kongwa imepandisha ufaulu kati ya Halmashauri 10, Halmashauri ya  Kongwa ni ya 6 Kitaifa katika matokeo ya mitihani ya darasa la saba 2024.


Awali, akitoa taarifa ya ufaulu kwa Halmashauri yake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Dkt. Omary Nkullo ameeleza kuwa matokeo ya kumaliza elimu ya msingi ufaulu umekua ukiongezeka tangu 2022 hadi 2024 ambapo umeongezeka kwa 13.21%  


Wilaya ya Kongwa imefanya sherehe hizo zilizokwenda sambamba na ugawaji wa zawadi za fedha taslimu kwa walimu na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari pamoja na tuzo kwa shule zilizofanya vizuri ikiwa ni motisha kwao kuzidi kujituma na kuendelea kuinua ufaulu zaidi na hatimaye kushika namba moja Kitaifa.





#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.