• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

UONGOZI WA C-FM RADIO WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA DODOMA

Imetumwa : September 12th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Staki Senyamule, ametembelewa ofisini kwake na uongozi wa Redio C- FM inayorusha matangazo yake kwenye Mkoa wa Dodoma, lengo kuu likiwa ni kujitambulisha pamoja na kufahamu matarajio ya Mkuu wa Mkoa katika kuutangaza Mkoa ambao pia ndio makao makuu ya nchi ya Tanzania.

Uongozi huo wa C-FM umeongozwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Redio Bwana Aloyce B.Ntukamazina pamoja na Meneja Mkuu wa Redio Bwana Dativus Mango ambapo sanjari na kujitambulisha kwa kiongozi wa Mkoa, wamepata fursa ya kujitangaza kwamba redio yao imejikita zaidi Vijijini ili kuweza kutatua kero za wananchi wa Dodoma.

Vilevile, wameanzisha miradi mbalimbali ambayo inaendelea kufanya kazi hasa katika utatuzi wa changamoto ya ukeketaji ambayo bado inaisumbua jamii ya wanadodoma ambapo wao kama chombo cha habari, wanatumika kama wahamasishaji kwa jamii kuweza kuachana na mila hizo potofu. Pia wameanzisha kampeni yenye lengo la kumkomboa mwanamke kutoka katika wimbi la unyanyasaji wa kijisia inayokwenda kwa jina la “Mwanamke Mwamba”

Mhe Senyamule ameupongeza uongozi wa redio hiyo kwa kuanzisha miradi hiyo ambayo itasaidia kuipatia jamii uelewa na kuamka kutoka kwenye mila potofu.

Akizungumzia mipango na matarajio yake kama Kiongozi wa Mkoa, Mhe Senyamule amesema kuwa ana matarajio na mipango mingi na mizuri kwa Dodoma hasa kwa kuwa ni makao makuu, unatakiwa ufanane na hadhi ya makao makuu. Kwa kuanza kwenye sekta ya miundombinu, tayari kuna miradi ya ujenzi inayoendelea kwa upande wa barabara za mzunguko / ring road, upanuzi wa barabara, ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato pamoja na soko kubwa la machinga.

Ameongeza kuwa, “tunaposema Dodoma ni makao makuu inatakiwa mpaka huko kwenye Halmashauri pafanane na hadhi hiyo na sio Jiji peke yake, kuwepo na Hoteli kubwa zenye hadhi ya nyota 5 katika Halmashauri zote pamoja na kumbi zitakazoweza kufanyika kwa vikao vya Kimataifa na ndio maana nimekuja na msemo wa, DODOMA, FAHARI YA WATANZANIA, STAWISHA DODOMA, WEKEZA DODOMA”. Amesisitiza Mhe Senyamule.

Aidha, Mkuu wa Mkoa amesema wananchi wa Dodoma hasa wanaoishi vijijini wanategemea Zaidi Kilimo ambapo ni asilimia 72 ya wanachi hao na zao kuu la Dodoma ni Zabibu japo bado halijafanyiwa matangazo ya kutosha kulinadi ili kuwezesha kupata masoko. Serikali inaonyesha dhamira ya dhati kuwekeza kwenye kilimo kama vile kwa sasa kuna miradi ya ujenzi wa mabwawa inayotarajiwa kuanza hivi karibuni katika Wilaya za Chamwino, Bahi na Mpwapwa.

Serikali inafanya Juhudi za kupata soko la uhakika kwa mchuzi wa Zabibu ambapo tayari imeshirikiana na Wizara ya Kilimo na kukubali kununua Tani 350,000 za mchuzi wa Zabibu kwa ajili ya Kiwanda cha Jambo kutengeneza Mvinyo pia maongezi yanaendelea na kiwanda cha Azam kwa ajili ya kutengeneza juice.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.