• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

“UTASHI WA MHE. RAIS KUTATUA MASUALA YA KODI NI MKUBWA “ BALOZI SEFUE

Imetumwa : January 20th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa kikao na Wafanyabiashara pamoja na wadau mbalimbali wa kodi Mkoa wa Dodoma chenye lengo la kukusanya maoni na kuyawasilisha kwa Mhe. Rais ili kupata muarobaini wa kudumu dhidi ya changamoto zinazowakabili walipa kodi nchini.

Kikao hicho kimefanyika leo Januari 20, 2025 kwenye ukumbi wa mikutano uliopo jengo la Safina Jijini Dodoma kikiongozwa na Mwenyekiti huyo ambaye alikifungua kwa kusema;

“Tunapokea maoni yenu kuhusu namna ya kuboresha mfumo wa kodi kwa sababu malalamiko mengi Rais ameshayasikia na alichotutuma ni kurudi kwake na mapendekezo ambayo hatuwezi kuyaandika sisi wenyewe,lazima tuwasikilize nyinyi wadau. Utashi wa Mhe. Rais kutatua masuala ya kodi ni mkubwa”Balozi  Sefue

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri, ameshauri;

“Kuwepo na namna mahsusi ya kikodi ya kuwaandaa na kuwawezesha wafanyabiashara wadogo waweze kushiriki katika uchumi shindani kwenye Makao Makuu ya Nchi, pia kufuatia ongezeko kubwa la watu, kuwe na ofisi mbili za kodi ili TRA iwe karibu zaidi na walipa kodi” Mhe. Shekimweri

Kadhalika, Katibu Tawala Msaidizi sekta za Biashara na Uwekezaji kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Mwajabu Nyamkomora ambaye alimuwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya, amesema;

“Mhe. Rais amesikia kilio cha Wafanyabiashara ndio maana ameunda Tume hii kwa ajili ya kusikiliza changamoto na kutoa mapendekezo ili kuhakikisha kwamba tunajenga mazingira ya kuwezesha biashara zetu zisonge mbele na kutoa ajira, kwani sekta binafsi ndizo zinazotoa ajira kwa wingi na zikiimarishwa zitaongeza pato la Nchi na familia”

Baadhi ya maoni yaliyopokelewa na tume hiyo kutoka kwa Wadau ni pamoja na; kupungua kwa utitiri wa kodi, kupanua wigo wa mlipa kodi, kuongeza idadi ya walipa kodi, Watendaji wa Mitaa wapewe elimu ya kutosha juu ya kodi kwani ndio wanaozungumza kwa karibu na Wananchi, Maafisa Kodi wawe na weledi kwenye utekelezaji wa majukumu yao.  

#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu                               #mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.