• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

VIONGOZI WA DINI WAASWA KUDUMISHA AMANI

Imetumwa : January 10th, 2023

VIONGOZI WA DINI WAASWA KUDUMISHA AMANI

Rai imetolewa kwa Viongozi wa dini wa Mkoa wa Dodoma kusisitiza amani hasa kipindi hiki ambacho Serikali imeruhusu kuanza kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa iliyokua imezuiliwa kwa takribani miaka saba. Kupitia kikao hicho viongozi wa dini wa mkoa wamejadili mustakabali wa amani kwa mkoa wa Dodoma katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi yake Jengo la Mkapa.

Akizungumzia suala la kudumisha amani, Mhe. Senyamule amesema; “Serikali ya awamu ya sita imeazimia mwaka huu uwe wa kutunza na kudumisha amani. Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa hivyo nitoe wito kwa viongozi wa dini kuhubiri amani kwa waumini wenu huko kwenye nyumba za ibada kwani tunataka Mkoa wetu ufanye mikutano hii kwa amani na utulivu”

Kupitia kikao hicho, viongozi hao wa dini walipata fursa ya kuwasilishiwa bajeti ya Mkoa kwa mwaka 2022/2023 ambapo Mkoa wa Dodoma umeidhinishiwa kiasi cha Shilingi 372,065,282,000 iliyogawanywa kwenye Halmashauri zake nane kwa matumizi mbalimbali ikiwemo miradi ya maendeleo inayoendelea kwenye Mkoa.

Katibu Tawala Mkoa Dkt. Fatuma Mganga amesema; “Tumeona ni vema viongozi wa dini mkashirikishwa kwenye matumizi ya bajeti ya mkoa kwani itakua rahisi kuwasilisha kazi zinazofanywa na Serikali kwa waumini wenu. Tutawaita tena kwenye wakati wa kupitishwa kwa bajeti ya mwaka huu mnamo mwezi Juni na tukimaliza mwaka pia tutawaita kuwapatia mrejesho”

Vilevile Katibu Tawala amegusia suala la elimu kwa kusema kuwa Serikali imetoa fedha za kujenga madarasa 940 kwa awamu zote mbili kwa mwaka 2022 hivyo wananchi wanapaswa kushiriki katika kujenga miundombinu ya elimu.

Amewataka viongozi hao kwenda kuhamasisha suala la uchumi kwa waumini wao kwa kuwa jamii inaonekana kuwa na hali mbaya kiuchumi sababu zinazopelekea kushindwa kushiriki kuchangia nguvu kwenye masuala ya maendeleo hasa elimu. Amesema jamii ina wajibu wa kuisaidia Serikali kwani haiwezi kutekeleza kila kitu peke yake, wananchi wanapaswa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na miradi ya elimu.

Kadhalika, suala la rushwa limegusiwa kwenye kikao hicho hasa kwenye fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya Serikali na kupelekea Mkurugenzi wa TAKUKURU Mkoa Bw. Sosthenes Kibwengo kulizungumzia kwa kusema, “Suala la rushwa ni la kila mmoja wetu na ni muhimu tupate ushirikiano wa jamii ili kupambana nalo. Viongozi wa dini mnapaswa kuwa kioo kupinga rushwa. Sisi kama TAKUKURU, tunaahidi kusimamia vizuri fedha hizi za miradi ya mkoa na tumeanzisha program maalumu ya “TAKUKURU RAFIKI” ambayo itatusaidia kupambana na rushwa. Nitoe wito kwenu kupeleka program hii kwa wananchi wakatusaidie kuhamasisha kushiriki mapambano dhidi ya rushwa”

Naye Sheikh wa Mkoa Bw. Mustapha Rajab Shaaban akizungumza kwa niaba ya viongozi wa dini amesema “Tunaishukuru Serikali kwa kuruhusu mikutano ya siasa kwani viongozi wa dini kipindi cha nyuma tulikaa sehemu mbaya kwenye jamii kutokana na kuzuiwa kwa mikutano hiyo ila sasa tumewekwa huru. Tunawaasa viongozi wa siasa kuchunga amani ya nchi na pia watumishi wa Serikali wathamini viongozi wa dini”

Kikao hicho kilichohudhuriwa na Katibu Tawala Mkoa Dkt. Fatuma Mganga pamoja na viongozi wa Taasisi na Idara, kililenga kuwashirikisha viongozi wa dini mambo mbalimbali yanayofanywa na Ofisi ya Mkoa na kilitawaliwa na ajenda kubwa ya namna ya kutunza maadili kwa watoto na vijana kwenye jamiii, uwasilishaji wa bajeti ya Mkoa na matumizi yake kwa mwaka uliopita, suala la elimu, kilimo pamoja na utunzaji wa mazingira.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.