• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

VITUO VYA HUDUMA ZA AFYA 235 MKOA WA DODOMA VYAPATIWA VIFAA VYA TEHAMA

Imetumwa : September 11th, 2024

 Vituo 235 vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Dodoma, vinatarajiwa kunufaika na vifaa vya Mradi wa kupanua matumizi ya Mfumo wa utoaji huduma za Afya Serikalini (GOTHOMIS) katika Mkoa wa Dodoma vilivyotolewa na Serikali ya Korea kupitia Shirika la KOICA linalotekeleza mradi huo Mkoani hapo. 

 Hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule, imefanyika leo Septemba 11, 2024 kwenye ukumbi wa ofisi yake, jengo la Mkapa Jijini Dodoma ikihudhuriwa na wawakilishi kutoka Wizara ya afya na TAMISEMI.

Akitoa Hotuba yake katika hafla hiyo, Mkuu huyo wa Mkoa ametoa wito kwa Mganga Mkuu wa Mkoa na wale wa Wilaya juu ya utunzaji wa vifaa hiyo vilivyotumia gharama kubwa kwa ajili ya kupanua matumizi ya Mfumo wa GOTHOMIS katika Mkoa wa Dodoma.

 “Vituo 135 vitapata vifaa hivi vikiambatana na usimikaji pamoja na mafunzo kwa watumiaji, vituo 82 vitapewa vifaa pekee hivyo, Wakurugenzi hakikisheni vifaa hivi vinasimikwa na kuanza kutumika ili tusipoteze dhamira ya waliotuwezesha. 

 “Mganga Mkuu wa Mkoa na waganga wa Wilaya, simamieni matumizi ya vifaa hivi na vitumike kwa mujibu wa watengenezaji. Watu watakaotumia mfumo wawe watu sahihi, makini, waadilifu, wenye utashi na uzalendo mkubwa”

Amesisitiza Mhe. Senyamule. Kadhalika, Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI Dkt. Grace Maghembe, amesema Serikali ya awamu ya Sita imekua ikisisitiza Matumizi ya Mifumo ili kuondoa ukiritimba kwenye utoaji huduma pia mfumo utapunguza mianya ya rushwa na matumizi mabaya ya fedha lakini kikubwa ni kuboresha huduma kwa wananchi. 

 Naye, Mkurugenzi Mkaazi wa KOICA Bw. Man Sik Shin, amesema Serikali yake inashirikiana na Tanzania kwenye utekelezaji wa miradi ya sekta za elimu na afya ambapo Mradi huo umegharimu kiasi cha dola Milioni 6.2 na baadhi ya vifaa walivyokabidhi ni kompyuta, kompyuta mpakato, seva na vishikwambi kwa ajili ya matumizi ya mfumo wa afya.

 Mradi huo unalenga kwenye ununuzi na usimikaji wa vifaa vya kutolea huduma za afya, kusaidia usimikaji wa GOTHOMIS kwenye vituo hivyo, kuwajengea uwezo watumiaji wa mfumo na wataalam wa TEHAMA OR-TAMISEMI pamoja na kutoa ushauri wa kuboresha Mfumo huo.   


   #dodomafahariyawatanzania #keroyakowajibuwangu












ReplyForward


Add reaction










Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.