• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AFURAHISHWA NA KASI YA UJENZI WA KIWANDA CHA MBOLEA

Imetumwa : December 21st, 2022

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea ujenzi wa kiwanda cha mbolea cha ITRACOM kilichopo kata ya Nala mkoani Dodoma na kupongeza kasi ya ujenzi wa kiwanda hicho huku akiwataka wananchi kuchangamkia fursa za ajira zilizopo kiwandani hapo.

Akizungumza na wananchi wa kata Nala mkoani Dodoma Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanzia Mhe. Kassim Majaliwa ameipongeza Wizara ya Kilimo kupitia Waziri wake Mhe. Hussein Bashe kwa kuhamasisha agenda ya uwekezaji kwa  kuleta mapinduzi makubwa ndani ya sekta ya kilimo kwa kujenga kiwanda hicho ndani ya mkoa wa Dodoma.

Pia Waziri Majaliwa amewataka wakazi wa Dodoma kuchangamkia fursa za ajira na ujasiriamali katika kiwanda hicho ambacho mpaka sasa kina jumla ya wafanyakazi 972 na kinatarajiwa kuwa na idadi ya wafanyakazi zaidi ya 4,000 ifikapo mwaka 2023.

Aidha Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe ameipongeza bodi ya kiwanda hicho kwa kuwa na wataalamu mbalimbali wanaohakikisha ubora wa mbolea hiyo kwakuzingatia mahitaji ya wakulima na kusema kuwa Wakulima watanufaika na mbolea ya ruzuku kwakuwa kiwanda hicho kimeanza uzalishaji na kinatarajia kuzalisha tani milioni 1 pindi kitakapo zinduliwa mapema mwezi Septemba 2023.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema kiwanda hicho kikubwa ndani ya mkoa wa Dodoma kitaleta tija kwa Wakulima wa Jiji la Dodoma na Tanzania kwa ujumla.

“Serikali tayari imekwisha toa agizo kwa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Kujenga barabara yenye urefu wa kilometa saba kwa kiwango cha lami kwa ajili ya kurahisisha shughuli za usafirishaji katika kiwanda hicho, pia kuwezesha upatikanaji wa maji kwa kuchimba visima vyenye thamani ya shilingi bilioni 7 pamoja na kumwongezea mwekezaji ekari 50 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za wafanyakazi, Kiwanja cha mpira pamoja na Kituo cha Polisi, ujenzi utakaoanza mapema Januari 2023” alisema Mheshimiwa Senyamule.

Mkoa wa Dodoma unatarajiwa kuongeza uzalishaji wa chakula pindi kiwanda hicho kitakapo kamilika mwaka 2023 kwakuwa kitasaidia wakulima kupata mbolea kwa bei nafuu na kuleta kilimo chenye tija.

ITRACOM FERTIZERS LTD ni Kampuni ya kuzalisha mbolea za FOMI (Mseto wa mbolea za asili ikiwemo samadi na mbolea za chumvichumvi). Kampuni hii imeanza uzalishaji wa aina tatu ya mbolea ya FOMI ambazo ni FOMI Otesha, FOMI Kukuzia na FOMI NENEPESHA  na kiwanda hiki kinatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi Septemba 2023.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.