• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAHITIMU TUMIENI ELIMU ZENU KUONGEZA TIJA SERIKALINI RC -SENYAMULE

Imetumwa : December 16th, 2023

Serikali imeahidi kuendelea Kushirikiana na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)Tawi la Dodoma katika kutatua changamoto mbalimbali kwa kuwa na wafanyakazi wenye ujuzi na weledi wa kutosha kuhudumia Watanzania.

Kauli hiyo imetolewa  na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule wakati akitoa hotuba yake kwenye Mahafali ya 49 ya Chuo cha IFM yaliyofanyika Disemba 16,2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa St.Gaspar Jijini Dodoma.

"Serikali inaahidi kuendelea Kushirikiana na Chuo cha Usimamizi wa Fedha katika kutatua changamoto mbalimbali, lengo ni kuhakikisha kuwa chuo kinakuwa kwanza wafanyakazi wakutosha wenye ujuzi na weledi kutosha kuhudumia Watanzania pili kuwa na miundombinu ya kutosha  kuendelea kuhudumia Wanafunzi waliojiunga katika chuo hicho na pia chuo kuendeleza majukumu yake kwa ufanisi".

Aidha ,Mhe.Senyamule amewataka wahitimu na Chuo kwa ujumla kujitathmini juu ya elimu iliyotolewa na waliyoipata kuona ni namna gani inatumika kuongeza tija Serikalini na hata katika soko la Dunia hasa katika Zama hizi za Utandawazi.


Kwa upande wake ,Mkuu wa chuo hicho cha Usimamizi wa Fedha Prof .Josephat Loto   ameainisha changamoto zinazozikabili chuo hicho ikiwemo ukosefo wa mabweni, uhababa wa watendakazi na gharama za kupangisha na kuomba Serikali katika utatuzi wa hayo.

Prof. Loto ameongeza kuwa chuo hicho kimefanya ushirikiano na vyuo vya Kimataifa 12  ili kuwapa wahitimu vionjo vya Kimataifa.

"Pia Mgeni Rasmi Chuo chetu tunafanya Mashirikiano na Vyuo vya Kimataifa 12 Nchi mbalimbali ikiwemo Ulaya, Asia na Afrika ya Kusini ikiwa lengo ni kuwapa wahitimu vionjo vya Kimataifa"

Naye ,Mwenyekiti wa Baraza la chuo Prof. Emmanuel Mjema  ameiomba Serikali kusaidia katika eneo la ujenzi ili waweze kujenga majengo makubwa na mazuri yanayoendana na hadhi ya Chuo na makao makuu ya Chama na Serikali.

"Tunaomba msaada wa Serikali ili tujenge majengo makubwa na mazuri yanayoendana na hadhi ya Chuo cha IFM na makao makuu ya Chama na Serikali katika eneo letu kubwa lililopo eneo la Nala".

Haya ni Mahafali ya 49 ya Chuo cha IFM yaliyojumuisha wahitimu 121 wanawake wakiwa 60 na wanaume wakiwa 61, ambapo Astashahada wahitimu ni 55, Stashada wahitimu 23 na Shahada ya Uzamili ni wahitimu 43.


Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.