• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAKAZI WA BUSI - KONDOA WATAHADHARISHWA JUU YA UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI

Imetumwa : May 14th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Wananchi wa Kata ya Busi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa wametakiwa kuchukua tahadhari juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji, kwani kwa sasa maji yanazidi kupungua kutokana na ongezeko la watu kila uchao lakini maji hayaongezeki.

Tahadhari hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule Mei 13, 2025 alipokua akizungumza na wananchi hao wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mahakama ya mwanzo ya Kata hiyo baada ya kutolewa kero ya ukosefu wa maji.

“Tunapoelekea maji yatazidi kupungua, na wenzetu wanatuambia vita kubwa Duniani itakayokuja ni kugombania maji.Kama tusipochukua tahadhari leo kuanza kutumia maji kwa vipimo, kutumia maji kwa tahadhari kutunza vyanzo vya maji ili yasipungue kwa sababu watu tunaongezeka kila siku lakini maji ni yaleyale. Hili jambo lipo mikononi mwenu”.

Aidha, Meneja RUWASA Wilaya ya Kondoa Mhandisi Loini Merinyo, amesema changamoto kubwa inayoikabili Kata hiyo ni wizi wa miundombinu ya maji hasa koki za kufungulia matenki ya kuhifadhia maji ambazo zimekua zikiibiwa kila zinapowekwa hali inayosababisha upotevu wa maji kwa kiasi kikubwa.

Awali, Mkuu wa Mkoa alitembelea mradi wa ujenzi wa nyumba nne za walimu katika shule ya msingi Foe iliyopo katika Kata ya Kalamba Halmashauri ya Kondoa ikiwa na jumla ya wananfunzi 402 wakiwemo wavulana 199 na wasichana 203 huku ikiwa na walimu watano walioajiriwa na wawili wakujitolea.

Mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 201.9 kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania na upo kwenye hatua za umaliziaji ambapo unatarajiwa kumaliza changamoto ya upungufu wa nyumba za walimu shuleni hapo hali itakayosaidia kuimarisha utoaji wa huduma ya elimu kwa wanafunzi wa Kata hiyo.

Akiwa shuleni hapo, Mhe. Senyamule alipata fursa ya kuzungumza na Wazazi pamoja na Wanafunzi wa shule hiyo amesema kuwa uongozi wa Mkoa na Wilaya hiyo utahakikisha unaangalia namna ya kushughulikia mradi huo ukamilike haraka ili Walimu wafaidike kama ambavyo Mhe. Rais alikusudia.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyaangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.