• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAKAZI WA NTYUKA WANUFAIKA WA MAJISAFI-DODOMA

Imetumwa : June 2nd, 2023


Naibu Waziri Wizara ya Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka bodi ya tisa ya Maji kuendelea kuboresha maslahi na kutatua changamoto ya upatikanaji wa Maji kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma kwani ndio kazi kubwa ya Wizara ya Maji ili kuhakikisha kufikia dhamira ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo Kichwani inafanikiwa Kwa asilimia 100.

Mhandisi Mahundi amesema hayo leo Juni 1,2023 wakati akimwakilisha Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso kwenye hafla ya uzindua wa mradi wa maji safi eneo la Ntyuka Chimalaa na bodi ya tisa sambamba na kuaga bodi ya nane ya wakurugenzi ya Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Dodoma ilifanyika katika Ofisi za DUWASA jijini humo.

"Niwapongeze Mwenyekiti na Bodi nzima mpya uteuzi wenu unaonyesha imani ambayo Wizara inayo juu yenu ili muweze kisimamia vyema Menejimenti pamoja na watumishi wote wa DUWASA na kuendelea kuimarisha utendaji ilikuweza kupata matokeo yanayo tarajiwa katika nchi yetu "amefafanua Mahundi

Aidha ,Mheshimiwa Mahundi katika Uzinduzi huo ameitaka DUWASA kufikisha maji katika Zahanati ya Ntyuka ili kuhakikisha huduma ya maji inapatikana na wakina mama wanapokwenda kujifungua wapate maji ya kutosha.

"Dhamira ya Dkt.Samia ni kuhakikisha huduma ya maji inafika Kwa asilimia 100 katika maeneo ya yanayotoa huduma za kijamii ikiwemo kwenye vituo vya Afya hivyo basi Mkurugenzi Wa DUWASA nakuagiza kahakikishe huduma ya maji inafika kwenye Zahanati ya Ntyuka,"amesema Mahundi

Kwa Upande Wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amewapongeza Wizara ya Maji na timu nzima ya mamlaka ya maji Dodoma DUWASA kwa kuendelea kuimarisha huduma ya Maji ndani ya Mkoa hadi kufikia angalau nusu ya mahitaji yanayohitajika pamoja na ongezeko la watu katika jiji hilo.

"Tunafurahi kumekuwa na ongezeko la maji pamoja na uzinduzi wa miradi mbalimbali inayoendelea kuzinduliwa zote hizo ziko ndani ya matumizi ya maji hivyo naipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuimarisha wizara hii kulingana na ongezeko linalo endelea la watu katika Mkoa huu " ,Amefafanua Senyamule

Awali akitoa Taarifa ya Mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majasafi na Usafi wa Mazingira (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph,amesema kuwa Mradi huo utawanufaisha wakazi zaidi ya 4,441 katika maeneo ya Ntyuka mtaa wa Chimalaa na Nyerere ambao Kwa sasa watapata maji Kwa asilimia 97 kutoka asilimia 0 ya awali kwa gharama za Mradi huo Kwa awamu ya kwanza mpaka kufikisha maji Kwa wananchi ambao ndio walengwa imefikia zaidi ya Shilingi Milioni 471.



Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.