• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAKULIMA WA ZABIBU MAMBO BAM BAM

Imetumwa : November 14th, 2024


Na.Sizah Kangalawe 

Habari- Dodoma Rs

Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma lenye dhima ya kuangalia, kujadili na kuandaa mipango mikakati mbalimbali ya kukuza Biashara Mkoani Dodoma, limefanyika Novemba 14/ 2024 ikiwa  ni baraza la kwanza katika mwaka wa Fedha wa 2024/2025.

Kikao kazi cha Baraza hilo kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jengo la Mkapa ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amepata wasaa wa kuwasihi wafanyabiashara na wawekezaji wa Mkoa huu kuwekeza katika biashara ya malazi na chakula hususani katika maeneo ya pembezoni mwa Stesheni ya Mwendokasi iliyopo Mkonze Jijini Dodoma.

‘’Tangu Treni imeanza kufanya kazi watu zaidi ya 3000 wanaingia  Dodoma kila siku ndio waende Mikoa mingine, nyie wafanyabiashara tumieni fursa ya kujenga mahoteli, lodge na Migahawa kwasababu uhitaji wa huduma hizo kwa maeneo yale ni mkubwa na bado watu hawajatumia fursa hiyo vizuri.

Aidha Mhe. Senyamule ameweka bayana uwepo wa soko zuri la zabibu lililosababisha kuwaondoa wakulima katika kadhia ya zao hilo adhimu kuharibikia mashambani kutokana na kukosa masoko.

‘’Miaka miwili nyuma tulikuwa na viwanda visivyozidi 8 vya Zabibu lakini leo tunapoongea tuna viwanda zaidi ya 38 vya kuongeza thamani ya  zabibu, nyie ni mashahidi mwaka huu hatujapata mtu wa kulalamika zabibu zimeoza shambani lakini nasikia watu wanaosema zabibu hazitoshelezi kutokana na kukua kwa mahitaji ya zao hili.

Kupitia vikao hivi tuangalie namna ya kuongeza uzalishaji kwasababu watu wamegundua kuwekeza sio lazima uwe na kiwanda kikubwa ila kupitia viwanda vidogo vidogo inawezekana na inaleta tija kwa wakulima’’, amesema Senyamule

Kwa upande wake katibu mtendaji wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania- Dodoma Bw. Alexander Mallya ameiomba Serikali kuweka katika kapu moja ushuru na tozo mbalimbali wanazotakiwa kuzilipa  ili kuepusha usumbufu mdogo mdogo unaotokana na kufuatwa na maafisa wa serikali wanaofanya kazi ya kukusanya tozo na ushuru huo kwenda kwa nyakati tofauti.

Hatahivyo kwa mujibu wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) tangu Mwaka 1987 - 2024, Miradi ya uwekezaji zaidi   ya 210 imetekekelezwa katika Mkoa wa Dodoma na kusababisha  ajira 28,703 kwa wakazi na wananchi wa Mkoa huu.


#dodomafahariyawatanzania

#dodomatupotayarikupigakura

#kurayakosautiyako

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.