• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WALIMU SIMAMIENI WANAFUNZI KUTUMIA MAKTABA MHE SENYAMULE

Imetumwa : January 24th, 2024

Wito umetolewa kwa walimu wa shule ya sekondari Mnadani kuwaelekeza wanafunzi namna nzuri ya kutumia Maktaba ili kupata matunda mazuri kwenye matokeo ya mitihani ya mwisho.

 Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Leo Januari 24, 2024 alipokua akizindua Maktaba ya kujisomea iliyojengwa na Taasisi ya Genesis for Children Organization kwenye shule ya sekondari Mnadani inayopatikana kwenye Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Mhe. Senyamule amesisitiza kuwa uwepo wa Maktaba hiyo uwe chachu kwa wanafunzi kusoma kwa bidii na kuongeza maarifa na utashi.

"Suala la shule linahusisha wadau pia na si Serikali peke yake ndio maana Genesis wameliona hilo. Mkoa wa Dodoma una shule za Sekondari 250. Dodoma Jiji ina shule 42 lakini kati ya hizo ni shule 9 tu ndizo zina Maktaba kwa ajili ya wanafunzi kujisomea na kujifunzia. Hongera kwa shule ya Mnadani kupata bahati hii ya kuwa shule ya pili kupata Maktaba.

"Nitoe Wito kwa walimu kuwasaidia wanafunzi waweze kutumia vizuri Maktaba hii ili kupata ujuzi, maarifa na utashi kwani Serikali imefanya uwekezaji Mkubwa kwenye sekta ya Elimu na Genesis wametusaidia pia. Natarajia kuona matokeo mazuri kwa kidato cha 4 mwaka huu kwani ninaamini hayatofanana na ya mwaka jana kama ambavyo Genesis wanashuhudia kupitia matokeo ya shule ya kwanza kujenga Maktaba kama hii" Mhe. Senyamule 

Nae Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jiji Mhe. Jabir Shekimweri amesema uwepo wa Maktaba hiyo utasaidia wanafunzi kufanya rejea ya vitabu vya ziada na kiada. Hii inajenga uzalendo kwa watoto kufahamu kazi kubwa inayofanywa na Serikali yao kupitia kusoma magazeti na machapisho mbalimbali yanayohofadhiwa hapo.


Kadhalika, Mkurungenzi wa Genesis Bi. Irene Kitoti wakati akisoma hotuba yake mbele ya mgeni rasmi, amesema Maktaba hiyo ni ya pili kujengwa kwa Tanzania Bara tangu kuanza kwa mradi na imegharimu kiasi cha shilingi Milioni 18.9 . Ameongeza kuwa Maktaba hiyo itafungua ufahamu wa wanafunzi na kitimiza malengo yao.


Taasisi ya Genesis for Children Organization ilianza rasmi mwaka 2022 na ilipata usajili tarehe 10/05/2023 ikiwa na lengo la kuchangia ukuaji wa Elimu kwa ngazi ya msingi na sekondari kwa kujenga Maktaba zitakazosaidia wanafunzi kujisomea na kujifunzia kwa kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI na mpaka sasa wameshajenga Maktaba 3, 2 Tanzania Bara na 1 Visiwani Zanzibar.













ReplyForward


Add reaction










Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.