• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WALIMU WA MASOMO YA HISABATI NA KIINGEREZA DODODMA WANOLEWA

Imetumwa : March 13th, 2025



Na.Francisca Mselemu

       Habari - DODOMA  RS


Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mkoa wa Dodoma Mwalimu Vincent B. Kayombo leo Machi 13, 2025 amefungua mafunzo ya siku mbili kwa walimu wa masomo ya Kiingereza na Hisabati katika ukumbi wa Mikutano wa Kondoa Irangi uliopo wilayani Kondoa.


Akizungumza kwenye hotuba yake Mwl. Kayombo amesema; "Shule Bora wamekuwa wadau muhimu katika kushirikiana na Serikali kuinua kiwango na  ubora wa elimu kwa kutoa mafunzo kwa walimu.


Mwenendo wa ufaulu  wa Mkoa wa Dodoma ni mzuri kwani katika mitihani ya Taifa ya darasa la Saba mwaka 2024 Mkoa ulifaulisha kwa 87.89% kwa kushika nafasi ya 4 kati ya mikoa 26 ya Tanzania Bara, kadhalika katika  upimaji wa Kitaifa wa darasa la Nne, mkoa ulifaulisha kwa 94.64% na ulishika nafasi ya tatu Kitaifa.


Kwa upande wa Sekondari Mkoa umepandisha ufaulu, idadi ya wanaofanya vizuri kidato cha Pili na cha Nne kwa ufaulu wa  daraja la Kwanza hadi la Tatu imeendelea kuongezeka kutoka 30% mwaka 2023 hadi 30.7% 2024.


"Hata hivyo pamoja na Mkoa kufanya vizuri, tuliona bado tuna jambo la kufanya, tulifanya tathimini na katika tathmini hiyo tulibaini changamoto mbalimbali, moja wapo ni baadhi ya Shule kutofanya vizuri kwenye masomo ya Kiingereza na Hesabu. Ninawapongeza na kuwashukuru Shule Bora kwa kukubali kutoa mafunzo haya”


Aidha, amewaasa Washiriki wa mafunzo hayo kutumia muda wao kujifunza, kwani anaamini watakapotulia  na kufuatilia mafunzo hayo kwa umakini, yatakuwa na tija kwao, Shule walizotoka na Mkoa kwa ujumla.


“Mnahitaji kuwa na ‘Proper attention’ mahali hapa pawepo na utulivu wa kutosha, hii sio semina ya kawaida. Mmekuja hapa kujifunza, kupewa uzoefu. Kinachotakiwa mseme kweli kwa dhati kabisa. Ukipewa nafasi ya kusema funguka. Hapa tumekuja kama wataalamu wa elimu, tuelekezane, ukiondoka na uliyokuja nayo, hujatupatia yale mazuri hujatusaidia sisi wala Mkoa.


Katika hatua nyingine Kayombo amewaagiza Maafisa Elimu (W) kuhakikisha  wanakwenda  kuwatumia walimu walioshiriki mafunzo hayo kuwapatia walimu wengine maarifa watakayoyapata. Na kwamba ana imani kubwa na Maafisa Elimu hao kwamba  watafanya bidii, ambayo italeta matokeo chanya katika mitihani ya mwaka huu.


Mradi wa Shule Bora ulianza mwaka 2021 na utamalizika 2027, ukitekelezwa katika mikoa tisa ambayo  Dodoma, Mara, Pwani, Katavi,Tanga, Simiyu, Rukwa, Kigoma na Singida, chini ya ufadhili wa Serikali ya Uingereza kupitia ‘UK – Aid’.


Mafunzo yatafanyika katika mikoa yote ya mradi, Dodoma ni mkoa wa Nne kupatiwa mafunzo hayo ukitanguliwa na Tanga, Pwani na Kigoma.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.