• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WALIMU WATAKIWA KUWA MFANO KWA JAMII KWA KUTIMIZA WAJIBU WAO

Imetumwa : April 22nd, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Serikali ina matamanio makubwa ya kuona Walimu wanaendelea kuwa mfano kwa jamii inayowazunguka katika kutimiza wajibu wao wa msingi sambamba na majukumu mengine yanayoambatana na wajibu huo hususan kwenye masuala ya kusimamia Amani na Utulivu.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameyasema hayo wakati wa zoezi la uchaguzi wa Viongozi wapya wa Chama cha Walimu (CWT) Mkoa wa Dodoma watakao hudumu kwa kipindi cha miaka mitano (2025-2030) lililofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari ya Dodoma Aprili 22, 2025.

“Ni matamanio yetu sisi kama Serikali lakini matamanio ya Mkoa wa Dodoma kuona kuwa Walimu mnaendelea kutimiza wajibu wenu mkubwa wa msingi lakini mnaendelea kutimiza majukumu mengine kama mnavyopewa na muajiri wenu ambayo mnakua mkiyafanya wakati wote lakini pia, tunaendelea kutamani kuona walimu wanaendelea kuwa mfano bora katika jamii” Mhe. Senyamule.

Aidha, Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Mwalimu Vicent Kayombo, amesema kuwa ameshirikiana vyema na viongozi waliopita kwa kipindi cha miaka mitano na kupata mafanikio hivyo, yupo tayari kufanya kazi na viongozi wapya watakaochaguliwa kwa kuwa wote ni wakwake.

Hata hivyo, Msimamizi wa uchaguzi huo Bi. Yunis Tesha, amesema uchaguzi huo unatokana na muundo wa sheria ya kazi pamoja na Katiba ambazo zinaongoza uchaguzi hivyo, ana imani kuwa Wajumbe wote watafanya uchaguzi wa haki kwa maslahi ya Chama na kila mtu ana haki ya kupiga kura kwani ni demokrasia ya kila mmoja.

Nae, Mwenyekiti Mstaafu wa CWT Mkoa wa Dodoma Mwl. Samweli Malechela amesema kuwa, Uongozi wake umelinda hadhi na heshima ya Chama hicho kwa kufanya kazi kubwa ambapo bado Chama kina Wanachama wengi katika Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma tofauti na Mikoa mingine ambayo Wanachama wamegawanyika na kwenda kujiunga na vyama vingine


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

#karibumwengewauhuru2025mkoawadodoma

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.