• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WALIMUI WATAKIWA KUWEKA MSISITIZO WA MASOMO KUANZIA MADARASA YA CHINI

Imetumwa : March 13th, 2025

Na Francisca Mselemu      

      Habari - Dodoma RS


Walimu wametakiwa kuweka msisitizo  wa masomo kwa Wanafunzi kuanzia madarasa ya chini, badala ya ilivyo sasa ambapo wamekuwa wakiweka msisitizo kwa madarasa ya mitihani.


Hayo yamebainishwa na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Daktari Mjege Kinyota ambaye alikuwa mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo yaliyotolewa kwa Walimu wa masomo ya Kiingereza na Hisabati  ambayo yalifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kondoa Irangi uliopo Wilayani Kondoa mnamo Machi 13 na 14, 2025, ambapo amesema kuwa moja ya msisitizo waliouweka kwa walimu waliowapa mafunzo hayo ni kuhakikisha wanaweka msisitizo wa masomo kwenye madarasa yote.


“Suala jingine tulilolisisitiza sana, Walimu waache kusisitiza tu madarasa ya mitihani .Unapoanza  kuweka msisitizo  kwa Darasa la Nne na Darasa la Saba, wakati hukuweka msingi huku chini inaweza isitusaidie sana. Kwa hiyo tumesisitiza kwamba Walimu wakajenge msingi kuanzia chini. Kwa maana watoto wakijua kuhesabu, kusoma na kuandika katika ngazi ya chini, watakua na msingi mzuri ambao utawawezesha kufanya vizuri katika ngazi nyingine”.


Nao washiriki wa mafunzo hayo waliohojiwa kwa nyakati tofauti, walikuwa na haya ya kusema;

 “Kwanza nawashukuru Shule Bora  kwa kutuletea mafunzo haya, nitakwenda kuwapatia walimu wa masomo ya Hisabati na Kiingereza wa Halmashauri yangu ujuzi nilioupata, naamini kwa kufanya hivyo ufaulu katika masomo haya utaongezeka. Leticia Ndelwa, Afisa Elimu Taaluma Chamwino .


“Baada ya mafunzo haya, Mimi pamoja na walimu wote wa Kata yangu tulioshiriki, tutakwenda kuandaa  Jumuiya za Ujifunzaji, tutawaita walimu wote wa Hisabati na Kiingereza, tutawapatia ujuzi na uzoefu tulioupata wa namna nzuri ya kufundisha  ili kuweza kuinua ufaulu kwenye Halmashauri yetu. Emmanuel Lotto, Afisa Elimu Kata ya Buigiri.


“Matarajio yangu baada ya mafunzo haya, Mwalimu wa Shule yangu aliyeshiriki ataboresha mbinu za ufundishaji na ujifunzaji, lakini pia atajua namna gani anaweza kuwashirikisha wanafunzi zaidi kutokana na uzoefu ambao ameupata kutoka kwa walimu waliotoka Halmashauri nyingine”.

Hidaya Idowa, Mkuu wa Shule ya Msingi Makafa.


“Somo la Kiingereza ni pana, na ni lugha ngeni, lugha ngeni ina changamoto zake katika ujifunzaji, mafunzo haya yametupa ujuzi mpya, lakini pia kupitia kugawanywa kwenye makundi wakati wa mijadala tumeweza kukutana na walimu wengine ambao Shule zao zinafanya vizuri katika masomo haya, wametupa mbinu wanazozitumia, tumeshirikishana uzoefu” Emmanuel Kepha, Mwalimu wa Somo la Kiingereza Shule ya Msingi Mtumba.


“Msingi mkubwa wa kuliweza Somo la Hisabati ni kulipenda, watu wengi hawapendi hesabu kwa sababu ya  mtazamo uliojengeka miongoni mwa Jamii kwamba somo hili ni gumu, lakini sio gumu, mafunzo haya yametupa mbinu ambazo zitatusaidia katika ufundíshaji, mbinu hizo zitawafanya wanafunzi waelewe, lakini pia walipende Somo lenyewe. Kwa mbinu nilizozipata, Wanafunzi ninaowafundisha wataelewa vizuri zaidi, watalipenda Somo,na idadi ya wanaofaulu itaongezeka. Aidan Masima,Mwalimu wa Hisabati ,Shule ya Msingi Pwaga.


Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyowahusisha Maafisa Elimu Msingi, Maafisa Elimu Taaluma, Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule za msingi pamoja na walimu wa Masomo ya Kiingereza na Hisabati kutoka wilaya zote za Mkoa wa Dodoma, chini ya ufadhili wa UK- Aid kupitia mradi wa Shule Bora, ni muendelezo wa jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita ambayo tangu kuwepo kwake madarakani, imefanya uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Elimu, mafunzo ya mara kwa mara kwa Walimu pamoja na Wasimamizi wa Elimu yakiwa  sehemu ya uwekezaji huo.




#keroyakowajibuwangu

#wekezadodoma,stawisha

dodoma

#mtiwangu,birthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.