• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANANCHI WA SWAGASWAGA WAPEWA KILOMETA ZA MRABA 3880,KUPISHA PORI LA AKIBA

Imetumwa : November 8th, 2022

Katika kutimiza adhma ya kujitambulisha, kusikiliza kero za wananchi na kuwasilisha maelekezo ya Serikali kwa wananchi,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ambaye ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa Dkt. Fatuma Mganga, Kamati ya Ulinzi ya Mkoa na Wataalam Kutoka Ofisi ya Mkuu wa MKoa na Ofisi ya Kamishna wa Ardhi, ametembelea Pori la Akiba la Swagaswaga na kuzungumza na Viongozi na watumishi wa TAWA, Wakuu wa Wilaya za Chemba na Kondoa pamoja na viongozi wa Chama na Serikali na baada ya hapo kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Handa kilichopo eneo la karibu na Pori hilo.

Akizungumzia Pori la Akiba la Swagaswaga, Afisa Mkuu Mhifadhi Bw. Joseph Gagiri Reuben, ameeleza kuwa sehemu ya Pori la Akiba la Swagaswaga linapatikana katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba,Kondoa, Hanang na Mkoa wa Singida. Awali Pori hilo lilijulikana kama ‘Songs forest reserve 1959’ likiwa na ukubwa wa kilometa za mraba 871. Pori hilo linapakana na vijiji 17, ambapo kati ya hivyo vijiji 8 vipo wilaya ya Chemba, Vijiji 8 Kondoa na kijiji kimoja mkoa wa Singida.

“Pori hili lina faida nyingi kwani huchangia shughuli za uchumi, hulinda vyanzo vya maji ambayo ni muhimu katika ujenzi wa bwawa la Farkwa, utalii, doria, kuelimisha wananchi kuhusu uhifadhi, kufuatilia mitawanyiko ya wanyama (ikolojia. Awali tulikuwa tuna fanya utalii wa uwindaji na sasa tunataka kufanya utalii wa picha” Amesema Mhifadhi Gagiri Reuben.

Pamoja na faida za Pori hilo la akiba Mhifadhi Mkuu ameeleza kuwa wanakabiliana na changamoto mbalimbali zikiwa ni pamoja na uwepo wa Wageni Wachache ambapo wamejipanga kuboresha miundombinu, matangazo Na vipeperushi, Kushirikiana na tour operators, kuboresha mazingira ya uwekezaji, kuhamasisha utalii wa ndani. Changamoto nyingine ni kuendelea kuwepo na matukio ya kijangili hasa urinaji wa asali na uvunaji wa mbao- ambapo wanakabiliana na changamoto hiyo kwa kutumia taarifa za kiintelijensia, kuelekeza doria maeneo ya wanyama na uharibifu, wanashirikiana na viongozi wa vijiji na kamati ya ulinzi ya wilaya,kushauri na kuhamasisha upandaji wa miti na ufugaji wa nyuki. Uwepo wa matukio ya wanyama wakali Na waharibifu- ambapo wameendelea kufanya doria pamoja na changamoto ya migogoro ya mipaka ambapo kamati wa Mawaziri nane imeundwa ili kuja kushughulikia migogoro hiyo.

Aidha baada ya kikao hicho cha ndani Mkuu wa Mkoa amepata fursa ya kuongea na wananchi wa Handa ambapo amewaeleza kuwa lengo la ziara yake ni kusalimiana na kujitambulisha kwa wana Handa,pia kusikiliza kero na kuwapa maelekezo ya Serikali.

Hivyo kabla ya kuzungumza amewataka wananchi wa kijiji cha Handa kueleza changamoto zao ambapo wameeleza changamoto kubwa zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kero ya maji, kero ya shule kwani watoto wanataabika sana, hivyo wanaomba shule shikizi.Changamoto ya barabara angalau ya kwenda Singida na Wilayani zifunguliwe. Kuna baadhi ya wananchi wamenyang’anywa mifugo yao lakini mpaka sasa bado hawajalipwa fidia wala kurudishiwa mifugo yao japo waliahidiwa hivyo. Aidha Bw. Elikana Musa ameeleza kuwa mwaka 2013/2017/2021 nyumba zimebomolewa wametembea katika ofisi mbalimbali hawajapata majibu. Changamoto ya Josho la kuogeshea mifugo.

Akijibu Changamoto hizo, Mhe. Senyamule ameleza kuwa kuhusu suala la maji, Mkandarasi anatafutwa na kufikia Januari, 2023 kisima kitaanza kuchimbwa. Kuhusu changamoto ya Shule na Madarasa Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshatoa kiasi cha Tsh. 60 ml, 40ml na 25ml kwa ajili ya kujenga madarasa na kumalizia ambayo yalishaanza kujengwa. Aidha Mhe Rais ametoa kiasi cha Tsh. 50ml kwa ajili ya Ujenzi wa kituo cha afya na Tsh.7 9mln zipo njiani zinakuja kwa ajili ya Ujenzi wa madarasa.Kuhusu suala la dhuluma ya ngombe  ofisi husika kwa sasa inaendendelea na uchambuzi kwa kila aliyedhulumiwa ngombe zake, ili wale wenye haki  walipwe na warejeshewe ngombe zake.

“Rais Samia Suluhu Hassan anatamani Serikali yake iwe na fedha lakini fedha hiyo iwe fedha halali.Kuhusu suala la Josho la mifugo hili nalichukua,kilimo,mifugo na uvuvi”

Akizungumzia suala la Changamoto ya Mipaka kati ya Pori la Akiba la Swagaswaga na Kijiji cha Handa Mhe. Senyamule ameeleza kuwa Wananchi wengi wa Handa wanaishi ndani ya hifadhi. Kwa kuwa Serikli ya awamu ya sita ni Sikivu na inajali maslahi wa wananchi wake. Mhe Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kupokea taarifa ya kamati ya mawaziri nane, ameridhia wananchi wa Handa wapewe ardhi yenye ukubwa wa kilometa za mraba 3880. Ardhi hii itagawiwa kwa wananchi ambao maeneo yao yalikuwa yameingiliana  na Pori la Akiba la Swagaswaga ambayo ni Mnagana, Ilala A na Ilala B.Hivyo Hivi karibuni Watakuja wataalam  kutoka  TAWA wakishirikiana na wataalam wa Ardhi,watawagawia ardhi na mara baada ya hapo ndio watawataka wananchi kuhama.

“Hesha aliyotupa Mhe.Rais ni kubwa na huu ni utekelezaji wa ilani ya chama tawala.Hivyo kama sisi tumeheshimiwa hivyo na sisi lazima tuheshimu”. Amesisitiza Mhe. Senyamule.

Kuhusu changamoto ya mpaka wa Dodoma na Singida- tayari suala hili limeshafanyiwa kazi na kinachobakia ni Wakuu wa Mikoa kuonana na kuonyeshana mipaka kabla mwaka huu haujaisha.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.