• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANANCHI WAASWA KUTUNZA VYANZO VYA MAJI KWA VIZAZI VIJAVYO

Imetumwa : March 21st, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS


Rasilimali 'Maji', inatajwa kuwa bidhaa adhimu ambayo haina mbadala hivyo, kila Mdau anayehusika na utunzaji wa chanzo cha maji ametakiwa kuhakikisha rasilimali hiyo inatunzwa na kuwa endelevu kwa vizazi vyote kwa kuunga mkono juhudi za Serikali za utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti.


Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, alipokua mgeni rasmi kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa Programu shirikishi za uhifadhi wa rasilimali za maji katika hifadhi ya maji Bonde dogo la Makutupora Jijini Dodoma Machi 21, 2025.


Katika hotuba yake kwa Wadau na wakazi wa Kata ya Makutupora, Mhe. Senyamule amesema; "Tutambue kuwa rasilimali maji ni bidhaa adhimu ambayo haina mbadala hivyo, kila Mdau ana jukumu kubwa kuhakikisha rasilimali hii inatunzwa na kuwa endelevu kwa kizazi cha sasa na kizazi cha baadae.


"Sentensi hii tumeisikia mara nyingi lakini sina hakika kama watu wanaielewa. Kwani sisi leo tumekua waharibifu wa kukata miti bila kujali utunzaji wa mazingira. Ninyi ni wadau muhimu, ninawaomba muunge mkono juhudi za Serikali katika utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji ikiwemo kuomba vibali vya matumizi ya maji”. Ameongeza Mhe. Senyamule.


Aidha, Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma Mjini Bi. Sakina Mbugi, ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Jabir Shekimweri katika hafla hiyo amesema Wilaya yake inaendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuangalia namna bora ya kuhifadhi chanzo hiki kikuu cha maji kwa kuwa ndio tegemeo kwa Wilaya yake.


Nae, Mkuu wa Ofisi ya Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu Dodoma Muhandisi Noel Mushi, amesema, Bonde la Maji la Wami Ruvu limekua likifanya jitihada za utunzaji wa eneo hilo kwa kutoa elimu, kuweka alama za mipaka, mabango ya makatazo, kuchora na kusambaza ramani za eneo la hifadhi, kufanya tathmini ya eneo lililovamiwa na mengine kadhaa lengo likiwa ni kulifanya eneo hilo kuwa la kitalii.


Uzinduzi wa Program hiyo unalenga kuhamasisha utunzaji wa rasilimali za maji shirikishi ambazo zitalinda vyanzo vya maji na kunufaisha jamii zinazozunguka vyanzo hivyo. Hifadhi ya maji ya Bonde dogo la Makutupora, ni chanzo cha maji kinachotegemewa kwa sasa katika Jiji la Dodoma kwa asilimia 91.




#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.