• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANANCHI WAMEASWA KUFANYA MAZOEZI KUEPUKA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA

Imetumwa : February 13th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

Habari - DODOMA RS

Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama shinikizo la damu, saratani,kisukari na mengineyo, yametajwa kuendelea kua tishio Duniani kwani takribani vifo Milioni 41 sawa na 73% vinatokana na magonjwa hayo yanayoweza kuzuilika kwa watu kuhamasika kufanya mazoezi ya viungo kila siku ili kuutengenezea mwili Kinga dhidi ya maradhi hayo hatari.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, ameyasema hayo leo Februari 13, 2025 katika Maadhimisho ya siku ya Familia ya Polisi iliyoandaliwa na Jeshi hilo Mkoani hapa ambapo Mkuu huyo wa Mkoa alikua mgeni rasmi kwenye uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

"Takwimu zinaonesha kuwa vifo Milioni 41 sawa na 73% ya vifo vinatokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Lakini hapa Tanzania, magonjwa haya yanachangia 33% ya vifo vyote vinavyotokea. Nikimaanisha katika kila vifo vitatu, kimoja kinatokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza hivyo nitoe shime, wote tulioamua kuchukua hatua ya kufanya mazoezi, tuendelee kufanya hivyo kwani tutachangia kupunguza magonjwa hayo Nchini" Mhe. Senyamule.

Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma George Katabazi, amesema siku ya Familia ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma inayokwenda sambamba na Bonanza la michezo na burudani nyingine nyingi, imeandaliwa mahsusi kwa lengo la kuimarisha Afya ya mwili kupitia mazoezi na burudani ili kuendelea kuwa na Jeshi imara wakati wote kwa ulinzi wa Mkoa.

Hata hivyo, Mbunge wa Mchinga na mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Salma Kikwete nae ameungana na Jeshi hilo katika siku hiyo akilipongeza kwa kuandaa siku hiyo kwani inahamasisha ukakamavu kupitia mazoezi ya kutembea lakini pia inaimarisha umoja na upendo kupitia kushiriki michezo mbalimbali iliyoandaliwa.

Siku ya Familia ya Polisi Mkoa wa Dodoma ambayo imeshirikisha vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama Mkoa pamoja na klabu mbalimbali za mazoezi (jogging) zinazopatikana katika Jiji hili, ilianza na matembezi yaliyoanzia viwanja vya Chinangali, Nyerere square na hatimae uwanja wa Jamhuri, imeongozwa na kauli mbiu isemayo "Sisi ni Familia, Ushirikiano ni Nguzo Yetu".


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.