• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANANCHI WANATAKIWA KUUZA DHANA POTOFU UANDIKISHAJI DAFTARI LA MPIGA KURA.

Imetumwa : September 27th, 2024

Na Hellen M. Minja, Habari  - RS DODOMA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule, amewataka wananchi kupuuza dhana potofu juu ya zoezi la uandikishaji na uboreshaji wa daftari la kudumu la Mpiga kura linaloendelea kwenye baadhi ya Wilaya za Mkoa wa Dodoma kwamba kuna gharama zinazohitajika kufanikisha.

Mkuu huyo wa Mkoa ameyasema hayo wakati wa Mkutano na waandishi wa habari aliouitisha leo Septemba 27, 2024, kwenye ukumbi wa ofisi yake liliyopo jengo la Mkapa Jijini Dodoma kuzungumzia mchakato huo unaoendelea.

“Uandikishaji wapiga kura au uboreshaji taarifa za wapiga kura ni bure. Mwananchi hatakiwi kulipa fedha yeyote katika mchakato huu, dhana kwamba kuna gharama zinazohusiana na uandikishaji ni za uongo na zinapaswa kupuuzwa” Amesema Mhe. Senyamule

Aidha, ametoa ufafanuzi juu ya wananchi wenye vitambulisho vya zamani kwamba hawana sababu ya kujiandikisha upya kwani vitambulisho hivyo ni halali na vinaweza kutumika tena.

“Tunatoa ufafanuzi kwamba, vitambulisho vilivyotolewa hapo awali ni vitambulisho halali na vinaweza kutumika tena kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Hivyo basi, wananchi ambao walikwisha kujiandikisha huko nyuma, hawapaswi kuhofia kuwa vitambulisho vyao vimekwisha muda wake na hawahitaji kujiandikisha tena ili kupata kadi mpya” Mhe. Senyamule.

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa huyo ametoa ufafanuzi kuhusu uhusiano kati ya uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura na uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Mchakato huu wa uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura ni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, unafanywa ili  kuhakikisha kuwa kila Mtanzania mwenye haki ya kupiga kura, anapata nafasi ya kumchagua Diwani, Mbunge na Rais. Hauhusiani moja kwa moja na uchaguzi wa Serikali za Mitaa, taratibu zake za uandikishaji zilishatangazwa na Waziri Mwenye Dhamana”.

Mkoa wa Dodoma unakadiriwa kuwa na wapigakura 1,777,834, kati yao ambao hawajawahi kujiandikisha kwenye daftari ni 845,976. Vituo vya kuandikisha wapiga kura katika wilaya ya Dodoma ni 429, Bahi 191, Kongwa 229 na Chamwino ni 805.

#dodomafahariyawatanzania

#dodomatukotayarikujiandikisha

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.