• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANAWAKE VIONGOZI WA DODOMA WAJIPANMGA KUMPONGEZA RAIS

Imetumwa : November 2nd, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amefanya mkutano na wanawake viongozi wa Mkoa wa Dodoma kwenye ukumbi wa PSSSF ikiwa ni muendelezo wa utaratibu wake wa kuongea na makundi mbalimbali ya kijamii.

Lengo hasa la kufanya mkutano huu ni kusikiliza kero zinazolikabili kundi hili hususani wanawake ambao ndio wanabeba jamii kubwa ya watanzania. Kulingana na taarifa ya matokeo ya kwanza ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022. Tanzania ina jumla ya watu 61,741,120 ambapo kati ya watu hao 51% ni wanawake wakati wanaume ni 41%. Hali kadhalika idadi ya watu Mkoani Dododma ni watu 3,085,625 ambapo kati yao wanaume ni 1,512,760 sawa na 41% wakati wanawake ni watu 1,572,865 sawa na 51%.

Kupitia kikao hicho,Wanawake viongozi wa Mkoa wa Dodoma  wamepata fursa ya kuelezea kero zao ambazo zinawakilisha jamii nzima kama vile suala la mmomonyoko wa maadili kwa vijana, usafi wa mazingira,usafi na upandaji miti,ukatili wa wa kijinsia, elimu,utoro na mimba za utotoni, suala la uchumi kwa wanawake, afya ya mama na mtoto.

Baada ya kusikiliza kero hizo, Mkuu wa Mkoa amewaambia wanawake hao kuwa Mhe. Rais anatamani nafasi ya mwanamke itambulike katika uongozi ndio maana nafasi nyingi hivi sasa zinaongozwa na wanawake.

“Mhe. Rais anatamani wanawake wainuke na nafasi yao itambulike katika jamii ndio maana amewapatia nafasi nyingi za uongozi. Unapokuwa mwanamke, unatakiwa ufanye zaidi kuliko wanaume, ili kuonyesha uwezo mkubwa tulionao kwani wanawake tumejaliwa kufanya na kufikiria mambo mengi kwa wakati mmoja”  Amesisitiza, RC Senyamule.

Kadhalika, Mkuu wa Mkoa amewataka wanawake wawe tayari kushiriki katika kutatua kero hizo zilizowasilishwa kwani Serikali haiwezi kutatua kero zote hivyo tunapaswa kumsaidia Mhe. Rais katika kutatua ketro hizi za wananchi.

“Maafisa maendeleo ya jamii, muende mukaandae makundi sogezi tofauti kulingana na kero zilizopo na mupange watu watakaoshiriki kwenye kila kundi kwa ajili ya kujadiliana namna ya kumaliza tatizo hilo. Kila kundi lifanye kazi kwa malengo na mikakati na tuone ndani ya mwezi mmoja tumefanikiwa nini. Baada ya hapo, tutakutana tena kushirikishana mawazo yetu kwa kila kundi. Pia tutaunda kamati mbalimbali ambazo zitakuwa na jukumu la kumuongelea Rais kwa yale anayoyafanya kwa wananchi maana sio rahisi kwa wananchi wote kufahamu mambo mazuri anayoyafanya Rais wetu” Ameongeza

Akizungumza, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga, amesema wanawake wanapaswa kuwa tayari kupokea majukumu haya kwani yanawezekana kufanywa na wanawake.

“Tumeitwa hapa ili kupokea majukumu na kuyatekeleza il kuonyesha kwamba wanawake tunaweza katika utatuzi wa kero mbalimbali. Mfano tunaweza kujipanga kutatua suala la lishe kwa Watoto shuleni tunalitatua, kumaliza tatizo la Watoto wa mitaani na mengine kadha wa kadha. Naamini yote haya tunaweza.” Dkt. Mganga.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Mwanahamisi Munkunda amesisitiza suala la usafi kwa kusema Wanawake tunapashwa kutunza mazingira yetu kwa sababu serikali haiwezi kuja kufanya usafi majumbani mwetu.

Akizungumza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI,Mhe. Fatma Taufiq amesema “ Sisi wanawake wa Dodoma tupange namna nzuri yha kumpongeza Mhe. Rais, kwani amefanya mambo mengi sana ambayo tunatakiwa tuyasemee.

Akimalizia mweyekiti wa UWT   mkoa wa Dodoma, Bi. Neema Majule amesisitiza umuhimu wa kufanyia kazi Mikakati iliyotolewa, kama mwanamke  wa kisiasa,kiuchumi na kijamii,ili kujikwamua ni  lazima mikakati yote ifanyiwe kazi.

MWISHO.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.