• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WATAALAMU TATUENI KERO ZA WANANCHI TUZIMALIZE KABISA-RC SENYAMULE

Imetumwa : March 5th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS


Msisitizo umetolewa kwa Wataalam wanaohusika na masuala ya wananchi kuhakikisha wanatatua kero zao na kuzimaliza kabisa ili zisijirudie mara kwa mara pindi viongozi tofauti wa Serikali wanapofanya ziara kwenye maeneo yao ambayo wataalam hao walishayapitia.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amebainisha hayo wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua miradi ya maendeleo katika Kata ya Nzuguni Jijini Dodoma Machi 04, 2025 sambamba na kufanya mkutano wa hadhara na wananchi kwenye Ofisi za Kata ulioibua kero kuhusu  migogoro ya ardhi.


“Wataalam, tungetamani tukija hapa Nzuguni tukutane na kero mpya lakini sio zile ambazo tulishaambiwa na kuahidi kuzishughulikia. Nisisitize, tatueni kero za wananchi, tuzimalize kabisa. Tunatamani tusikie migogoro ya ardhi iliyotatuliwa  ikafika mwisho, kwani tangu kuanza program ya kusikiliza migogoro ya ardhi, kero hii imepungua kwa kiasi kikubwa”. RC Senyamule.


Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri amesema kuhusu masuala ya ardhi, kila kero iliyowasilishwa itolewe maelezo ya kina na ushahidi wa nyaraka na kuongeza kuwa hata wale watakaoleta kero zao kwa njia ya simu, kanuni itakayotumika ni hiyo hiyo ya ushahidi wa nyaraka.


Katika Mkutano huo, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Dkt. Fredrick Sagamiko, ametolea ufafanuzi kero za ardhi na kusema kuwa  Machi 05, 2025, Wataalam wa ardhi kutoka ofisini kwake wataweka kambi kwenye eneo hilo kusikiliza na kutatua kero zote zinazowakabili wananchi hao hivyo wafike na nyaraka zao bila kukosa.


Mbali na Mkutano huo, Mhe. Senyamule ametembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye Kata hiyo ikiwemo mradi wa sekta ya afya ambao ni ujenzi wa nyumba ya Watumishi wa Zahanati ya Kitelela (mbili kwa moja) ambao umekamilika kwa gharama ya shilingi milioni 60 na umeanza kutumika.


Miradi mingine iliyotembelewa ambayo imetekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri, ni ujenzi wa matundu 10 ya vyoo  katika shule ya Msingi Mahomanyika ambao umegharimu shilingi milioni 18, pamoja na ujenzi wa matundu 10 ya vyoo kwenye shule ya Msingi Nzuguni B uliogharimu shilingi milioni 20.


Ziara ilihitimishwa katika shule ya Sekondari ya Kata ya Nzuguni iliyoanzishwa mwaka 2007,ambayo kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 1344 ,mradi  unaotekelezwa  ni  ujenzi wa vyumba 4 vya  madarasa na ofisi kwa thamani ya shilingi milioni 129.5



#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.