• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WATAKWIMU WATAKIWA KUTOA TAKWIMU SAHIHI KWA VIONGOZI WAO

Imetumwa : November 21st, 2023

Rai imetolewa kwa watakwimu wa Halmashauri, Wizara, Idara naTaasisi za umma kufanya kazi ya ziada kwa kuwapatia viongozi wao takwimu sahihi ambazo zimepata kibali kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu pale wanapowasilisha taarifa kwa wananchi au viongozi wa juu ili kuepuka upotoshaji wa takwimu.

Hayo yamebainishwa leo Novemba 21, 2023 na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa wakati wa hafla ya maadhimisho ya 33 ya kilele cha siku ya Takwimu Afrika 2023 yaliyoandaliwa na Ofisi ya Takwimu Tanzania (NBS) ikishirikiana na Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika. ambapo hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya ofisi za Takwimu zilizopo Jijini Dodoma huku mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule.

"Watakwimu, tufanye kazi ya ziada kwa kuwapatia viongozi wetu Takwimu sahihi kwani wanaposimama mbele ya wananchi haipendezi kusikia kiongozi anataka Takwimu ambazo sio sahihi. Tuhakikishe Takwimu tunazowapatia viongozi wetu zimepata Baraka kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu kwani pale ndipo unapata Takwimu sahihi unazoweza kuzitumia sehemu yoyote," Amesisitiza Dkt. Chuwa Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazotoa Takwimu bora ulimwenguni pia ****ametaka**** umuhimu wa Takwimu kwa nchi za Afrika.

"Tanzania inatoa Takwimu bora zinazoaminika si Afrika tu Bali Dunia kwa ujumla. Mwaka 2010 Serikali ilitekeleza mradi wa Mpango kabambe wa Takwimu uliotekelezwa hadi mwaka 2018 na ambao uliimarisha upatikanaji wa Takwimu bora nchini, Nitoe Wito kwa Ofisi ya Mtakwimu msambaze taarifa kwenye Halmashauri zetu kwani Takwimu zinatakiwa kutumiwa kwenye kutafsiri mipango ya maendeleo kwa sekta zote. Takwimu zinasaidia nchi za Afrika kufahamu idadi ya rasilimali watu iliyopo na makundi yake," Mhe. Senyamule.

Hata hivyo, maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Kamisaa wa  Sensa kwa upande wa Zanzibar Balozi Mohamed Ally Hamza ambaye amesema maadhimisho hayo yana lengo kuu la kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu matumizi ya sensa pia ushirikishwaji wa jamii unasaidia kuongeza thamani ya Takwimu zetu. 

Maadhimisho ya siku ya Takwimu Afrika hufanyika Novemba 21 kila mwaka yakiwa na lengo la kuhamasisha matumizi sahihi ya Takwimu katika mipango ya nchi za Afrika kwani Takwimu zinahitajika wakati wowote.

Maadhimisho ya mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu isemayo "Uboreshaji wa mifumo ya ushirikiano wa kitakwimu ili kuharakisha utekelezaji wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA): Mchango wa Takwimu Rasmi katika mageuzi ya kiuchumi na maendeleo endelevu ya Afrika".













ReplyForward















Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.