• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WATALAAMU WA MAABARA ZA AFYA WARUHUSIWE KUHUDHURIA MAKONGAMANO - DKT BITEKO

Imetumwa : October 2nd, 2024

Na: Hellen M. Minja, Habari – DODOMA RS

Viongozi wa sekta za afya Nchini wametakiwa kuwaruhusu Wataalamu wa Maabara kushiriki kwenye Makongamano kwa mustakabali wa kuboresha utoaji huduma ya afya kwa Wananchi kwani taaluma hiyo ina thamani kubwa Nchini.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 02, 2024 na Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Dotto Biteko wakati akifungua rasmi Kongamano la 37 la Wataalamu wa Maabara ambapo amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

“Kumekua na tabia ya viongozi kutowaruhusu wataalamu hawa kuhudhuria Makongamano, Serikali inatambua na kuthamini mchango wa taaluma yao hivyo, kupitia Kongamano hili, nawataka viongozi wawaruhusu wataalamu hawa kushiriki na kusiwe na uzembe kwenye hili.” Amesema Dkt. Biteko

Naye, Waziri mwenye dhamana ya sekta ya afya Mhe. Jenista Mhagama, amesema Serikali imefanya maboresho kwenye sekta hiyo kwa kuongeza mashine za kiuchunguzi.

“Mhe Rais amefanya uboreshaji wa mashine za kiuchunguzi kama MRI, Ex–ray, Ultra sound na kuhakikisha huduma zinazotolewa na wataalamu hawa zinaendana na uboreshaji huu hivyo kupunguza wagonjwa wanaohitaji kwenda kupata matibabu nje ya nchi” Amesema Mhe. Mhagama

Aidha, akitoa salamu za Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule katika salamu zake amesema kipindi cha Serikali ya awamu ya sita kimeinufaisha Dodoma katika sekta ya afya.

“Dodoma tunavyo vituo vya kutolea huduma za afya 516, vituo vya kutolea huduma za maabara 217. Nitoe pongezi nyingi kwa Mhe. Rais kwa kuwezesha upatikanaji wa vifaa tiba pamoja na dawa kwa kiasi kikubwa kwani ametoa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 18.3 kuwezesha upatikanaji wa vifaa tiba na dawa” Mhe. Senyamule.

Akisoma risala ya Chama cha wataalamu wa Maabara za AfyaTanzania (MeLSAT), Rais wa chama hicho Bw. Yahya Mnung’a, ametaja changamoto ya utofauti wa mitaala ya kufundishia baina ya vyuo vya afya kuwa inazalisha wataalamu wa Maabara wasio na ufanisi.

“Taaluma ya maabara ina changamoto ambazo tunaamini zikifanyiwa kazi tutapiga hatua ikiwemo mkanganyiko wa mitaala ya kufundishia jambo linalopelekea kuzalishwa kwa wataalamu wasio na ushindani kwenye soko la ajira ndani na nje ya Tanzania”

Kongamano hilo la siku nne lililoandaliwa na MeLSAT, linashirikisha wataalamu wa maabara na wadau wa afya kutoka ndani na nje ya nchi ambapo lilianza Oktoba Mosi na litahitimishwa Oktoba 04, 2024 likiongozwa na kauli mbiu ya “zuia usugu wa dawa kupitia tafiti, ubora na matokeo ya kuaminika kutoka Maabara” 

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.