• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WATUMISHI KUWENI WAZALENDO MHE SENYAMULE

Imetumwa : July 14th, 2023

WATUMISHI KUWENI WAZALENDO-MHE.SENYAMULE

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewataka watumishi wote wa umma kuacha tamaa ya fedha za Miradi ya Serikali na kutanguliza utu na uzalendo mbele ili kujenga na kudumisha Uchumi wa Taifa. Amesema kila mtumishi wa Serikali anao wajibu wa kulinda fedha zote zinazotolewa kutekeleza Miradi Mbalimbali.

Senyamule ameyasema hayo wakati akihitimisha ziara yake ya kuzungumza na madiwani katika Halmashauri zote nane za Mkoa wa Dodoma kuhusu hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/2022, katika kikao kazi cha Baraza la Madiwani wa Jiji la Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma leo Julai 14/2023.

‘’Watumishi au wataalamu wa kada mbalimbali nyie ndio mmepewa dhamana ya kumsaidia Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa hiyo mnapopewa fedha za kutekelezea miradi na zikabaki kuweni wazi kwa kutanguliza uzalendo mbele na kuzitolea taarifa na kuzirejesha fedha hizo ili zitumike kufanyia jambo jingine lenye maslahi kwa wananchi wetu”.

Aidha katika kikao hicho Senyamule ameitaka Menejimenti ya Jiji la Dodoma kuhakikisha inaweka makisio sahihi ya vitega uchumi vyake pamoja na kuongeza kasi ya ukusanyaji wa Mapato ili kuongeza na kuimarisha uchumi wa Mkoa huo.

“Halmashauri ya Jiji inatakiwa kuwa na makisio sahihi ya vyanzo vyake vya vitega uchumi wake na ongezeni kasi ya makusanyo ili kuimarisha uchumi wa Mkoa kwasababu mnafahamu Jiji letu lina vitega uchumi vingi, tumieni fursa ya makao Makuu kuongeza mapato kwa kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza bila kuathiri mifumo ya kiutendaji” amesema Senyamule.

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri ameyataja mambo ambayo yakifanyika yanaweza kuondoa na kuepukana na hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuwa ni pamoja na kufuata kanuni, Sheria, Miongozo na Taratibu za Kazi, Mkaguzi wa ndani kufanya kazi kwa weledi na kufanya  kazi kwa uhuru  wake pasi na kuingiliwa na kuwa na Tume ndogo ya Watendaji wa kuthibiti hoja za mkaguzi Mkuu na Tume hiyo iwe na uwezo wa kuwawezesha na kuwajengea uwezo Wahasibu wa kujibu hoja mbele ya Mkaguzi Mkuu.

Katika vikao kazi vya Mkuu wa Mkoa na Mabaraza ya Madiwani wa Halmashauri za Wilaya, na Jiji la Dodoma, Mhe.Senyamule kwa nyakati tofauti amezitaja agenda za kudumu za Mkoa ambazo ni Mazingira, usimamizi wa Mapato ya Halmashauri, Elimu  ikiwa ni kukomesha utoro shuleni na kukuza kiwango cha ufaulu.    

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.