• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WATUMISHI WAASWA UPENDO,UADILIFU,KUFANYA KAZI KWA BIDII NA USHIRIKIANO

Imetumwa : October 26th, 2023


Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma, wameaswa kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano ili kuwezesha miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa na Halmashauri hiyo kuwa na tija na ufanisi mkubwa.

Rai hiyo imetolewa tarehe 25 Oktoba, 2023 na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw.Ally Gugu wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri hiyo yenye Lengo la kutathmini utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Mfanye kazi kama timu moja kwa kushirikianisha mambo na muwe na muunganiko na huo ndio upendo , taarifa za miradi zinapo Kuja mshirikishane isiwe ya mtu mmoja " ameeleza Gugu.

Aidha, Amesisitiza suala la usimamizi wa mapato ya Halmashauri na kusema ni lazima kusimamia kwa uaminifu fedha zikusanywe na kupelekwa sehemu husika pamoja na kutafuta mbinu nyingine za vyanzo vya mapato na zaidi ya yote ni kusimamia kwa uaminifu matumizi ya fedha za Serikali.

"Lazima muwe na mkakati madhubuti ya kusimamia mapato yaliyopo lakini kuzalisha vyanzo vipya vya mapato na kuvisimamia ,fedha zikusanywe na zipelekwe kwa wakati sehemu husika kwa kuzingatia sheria na taratibu za matumizi husika " Ameongeza

Katibu Tawala Mkoa pia amegusia suala la afya na kuwataka watumishi kuchukua tahadhari kwenye afua za maradhi ili kujiepusha na yale yanayo epukika pamoja na kuzingatia Lishe bora.

Kwa upande wake, Mkurungezi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpwapwa, Bi.Mwanahamisi Ally amemuahidi Katibu Tawala Mkoa kutekeleza maelekezo yote aliyotoa na kumuhakikishia kutoa taarifa kwa wakati.

Awali Bw. Gugu alianza na kikao cha pamoja cha tathmini ya miradi na vyanzo vya mapato ya ndani ya Halmashauri na Wakuu wa Idara kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na baada ya hapo alifika katika Shule mpya ya Sekondari ya Kimagai, Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa na Shule ya Sekondari ya Mazae kwa ajili ya ukaguzi na utekelezaji wa maendeleo ya miradi.

Pia, miradi hiyo mitatu kwa maana ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Kimagai, ujenzi wa Jengo la Huduma ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Wilaya, vyumba 9 vya madarasa, mabweni 4 na matundu kumi na manne ya vyoo unaogharimu zaidi ya shilingi Billioni moja.


Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.