• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WATUMISHI WATAKIWA KUJIKITA KWENYE MATUMIZI YA TEKNOLOGIA

Imetumwa : March 26th, 2025



Na.Hellen M. Minja,      

      Habari – DODOMA RS      


Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wametakiwa kujikita zaidi kwenye matumizi ya teknolojia ili kwenda sambamba na Dunia ya sasa, kwani hakuna njia mbadala ya kuepuka matumizi yake kwa kuwa kila kitu kinawekwa kwenye Mtandao.


Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule Leo Machi 26,2025 alipojumuika na Watumishi wake kushiriki chakula cha mchana  sambamba na kusheherekea kumbukizi za siku za kuzaliwa,kwa wazaliwa wa mwezi Machi,ambapo pia chakula hicho cha mchana  huambatana na utolewaji wa mada mbalimbali,mada ya leo ikiwa ni  matumizi ya Mfumo wa e Mrejesho.


“Kila mtu ashirikishwe kwenye teknolojia kwani ndio dunia inapoelekea na usiopoifuata itakuacha. Hakuna namna ya kuepuka matumizi ya TEHAMA, kila Mtumishi aingie kwenye matumizi hayo. Serikali yetu ina mifumo mingi hivyo jishirikishe ili uwe sehemu ya Dunia kwani kila kitu kinapelekwa kwenye mtandao” Mhe. Senyamule


Akitoa elimu juu ya matumizi ya Mfumo huo wenye lengo la kupata maoni ,malalamiko au pongezi juu ya huduma zitolewazo, Afisa Utumishi Mkuu wa Ofisi hii Bw. Gwamaka Mlagila amesema,


“e Mrejesho ni Mfumo wa kutuma, kupokea, kufuatilia malalamiko, maelekezo na pongezi. Ni jukwaa la kidigitali linalowezesha wananchi wa Tanzania kuwasilisha maoni, mabadiliko, mapendekezo au pongezi moja kwa moja kwa Taasisi za Serikali ili kuboresha uwazi, uwajibikaji katika utoaji huduma kwa Umma”.


Kwa Mkoa wa Dodoma, Mfumo huo utarahisisha utekelezaji kaulimbiu ya Mkoa ambayo ni “Kero yako, Wajibu Wangu”.




#dodomafahariyawatanzania                                

#keroyakowajibuwangu #mtiwangubirthdayyangu

[3/26, 19:52] Francisca Elimo: WATUMISHI WA DODOMA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA HADHI YA MAKAO MAKUU


Na. Hellen M. Minja,            

       Habari - DODOMA RS  


Watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wametakiwa kufanya kazi kuendana na hadhi ya Mkoa ambayo ni Makao Makuu ya Nchi ambapo watu wa aina mbalimbali wanapokelewa na kuhitaji huduma ndani ya Mkoa ambazo zinatakiwa kuwa tofauti kulingana na makundi yao.


Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipokua akifungua kikao cha mwaka cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika Machi 26, 2025 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jengo la Mkapa Jijini humu.


“Niendelee kusisitiza kupitia wahusika, Idara ya Utumishi, kuweka utamaduni kwa Watumishi wa Mkoa wa Dodoma kufanya kazi inayoendana na mazingira ya Dodoma hivyo huduma zetu zinatakiwa zioneshe utofauti wa makundi hayo tunayohudumia na ni wajibu wa kila Mtumishi kufahamu maono ya ofisi yake.”


Awali, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya amesema; “Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa mujibu kifungu cha 71 ina jumla ya Watumishi 198 lakini kwa sasa ina Watumishi 120, kwenye Wilaya wapo 78 lakini watumishi hao wanapaswa wawe jumla 303 hivyo kuna upungufu wa Watumishi 105 hasa kwenye ofisi za Wilaya”.


Ameongeza kuwa mwaka 2023, Ofisi yake katika kuwapata watumishi wote 303, ilifanya mazungumzo na Wizara husika ya Utumishi na kufanikiwa kupata ajira mpya 10 katika kipindi cha 2023/24 kulingana na kibali cha bajeti ya kipindi hicho na katika bajeti ya mwaka huu inayoendelea, imeomba ajira mpya 29.


Kadhalika Katibu Tawala Mmuya amesisitiza kufanyiwa kazi kwa hoja zote zilizowasilishwa katika  kikao cha baraza kilichopita huku akiweka mkazo  kwenye kulipwa kwa  stahiki za watumishi ambazo ni malipo ya likizo,makimbikizo ya mishahara,uhamisho  N.K.


Nae, Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dodoma Bi. Devotha Kiberenge, ameipongeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kutimiza dhana ya ushirikishwaji Wafanyakazi katika maamuzi kwani uwepo wa vyama hivyo mahala pa kazi unasaidia kuongeza tija kazini.


Baraza la Wafanyakazi limeundwa kisheria kupitia tamko la Mhe. Rais namba 1 la mwaka 1970 na Sheria ya Taasisi za kazi Sura namba 300 inayozungumza kuwepo kwa Mabaraza hayo lakini pia, Sheria ya mahusiano kazini Sura namba 366 ya mwaka 2019 hivyo ni muhimu kuwepo na hufanyika mara mbili kwa mwaka.




#dodomafahariyawatanzania                                

#keroyakowajibuwangu #mtiwangubirthdayyangu           

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.