• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAZIRI MKUU AZINDUA HUDUMA YA UAPANDIKIZAJI BENJAMIN MKAPA

Imetumwa : May 10th, 2023


WAZIRI  MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali iliamua kuwekeza shilingi bilioni 2.7 ili kuanzisha huduma ya upandikizaji uloto na kupunguza gharama za matibabu hayo kwa wananchi.

“Kwa lugha nyingine, kuimarika kwa huduma za kibingwa na bobezi nchini kumepunguza gharama kubwa iliyokuwa inatumiwa na Serikali ili kuwezesha Watanzania wenye uhitaji kupata huduma hizo nje ya nchi. Kwa mfano, huduma hii ya upandikizaji uloto ikitolewa katika hospitali hii, itagharimu shilingi milioni 50 hadi 55 kwa mgonjwa mmoja,” amesema. Amesema hayo leo (Jumatano, Mei 10, 2023) wakati akizungumza na wananchi na watumishi wa hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma mara baada ya kuzindua huduma za kibingwa za upandikizaji wa uloto (Bone Marrow Transplant) hasa kwa watu wenye Seli Mundu (Sickle Cell).

 Waziri Mkuu amesema Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa inakuwa hospitali ya pili baada ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuzindua huduma hiyo ya upandikizaji wa uloto na hivyo, kuifanya kuwa miongoni mwa hospitali chache zinazotoa huduma hiyo katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na Kati.

“Upandikizaji uloto unatoa nafuu kubwa sana kwa wagonjwa wa seli mundo kwani huwapunguzia kwa kiasi kikubwa maumivu na maambukizi ya mara kwa mara na wakati mwingine huwa sababu ya kupona kabisa kwa ugonjwa huu wa kudumu. Kutokana na nafuu hiyo, mgonjwa huweza kuishi maisha yenye ubora na kushiriki vema katika shughuli mbalimbali ikiwemo masomo”.

 Amesema uzinduzi wa huduma hiyo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa ni ushahidi tosha wa namna ambavyo Tanzania inapiga hatua kuboresha huduma za afya. “Huduma za namna hii kuendelea kutolewa katika hospitali zetu si jambo dogo, na hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa huduma kama hizi zinapatikana katika nchi chache sana kwenye bara la Afrika.” Katika hatua nyingine, Waziri Ummy amesema wizara hiyo inaangalia uwezekano wa kuipandisha hadhi hospitali hiyo ili iwe hospitali ya Taifa badala ya kuendelea kubakia kuwa ya kanda.

“Tumeanza kujenga kituo cha kutoa tiba ya kansa na pia tunataka tujenge kituo cha umahiri cha matibabu ya moyo ili kuimarisha utoaji wa huduma kwenye hospitali yetu.”

 Naye Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika alimweleza Waziri Mkuu kwamba tangu Januari 19, mwaka huu hadi leo, wamefanikiwa kupandikiza uloto kwa watoto watatu na wote wanaendelea vizuri.

“Watoto wawili wanatoka kijiji jirani cha Mapinduzi na mmoja anatoka eneo la Area D hapahapa Dodoma.”

 Alisema kufanyika kwa upandikizaji wa uloto kwenye hospitali hiyo, kumeifanya Tanzania iwe miongoni mwa nchi saba zinazotoa huduma hiyo barani Afrika. Alizitaja nchi nyingine zinazotoa huduma hiyo kuwa ni Algeria, Afrika ya Kusini, Misri, Morocco, Nigeria na Tunisia.

“Kwa mantiki hiyo, Tanzania inakuwa nchi ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kuanza kutoa huduma hiyo.” Kwa upande wake,

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Rosemary Senyamule amewapongeza watumishi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuhudumia wagongwa na ameishukuru Serikali ya Awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuimarisha huduma katika sekta ya afya na kuwasogezea wananchi huduma kwa karibu katika Mkoa wa Dodoma.

 Aidha ,Senyamule ametoa ahadi ya kuendelea kusimamia huduma bora katika majengo yote yanayo jengwa ndani ya Mkoa na kuhakikisha miradi hiyo inaisha kwa wakati ili kutekeleza dhamira ya fedha zilizo tolewa na serikali.

 "Nimpongeze Mkurugenzi wa Hospitali hii ya Benjamin Mkapa imekuwa sifa katika nchi yetu ya Tanzania wanakuja watu kutoka Mikoa mbalimbali lakini kinacho shanganza zaidi watu wanatoka Mkoa wa Dar-es-Salaam kuja kupata huduma huku " Kufuatia uzinduzi wa leo uliofanywa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Tanzania inakuwa moja kati ya nchi saba zinazotoa huduma hiyo barani Afrika.





















WAZIRI MKUU AZINDUA HUDUMA YA UPANDIKIZAJI ULOTO BENJAMIN MKAPA WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali iliamua kuwekeza shilingi bilioni 2.7 ili kuanzisha huduma ya upandikizaji uloto na kupunguza gharama za matibabu hayo kwa wananchi.“Kwa lugha nyingine, kuimarika kwa huduma za kibingwa na bobezi nchini kumepunguza gharama kubwa iliyokuwa inatumiwa na Serikali ili kuwezesha Watanzania wenye uhitaji kupata huduma hizo nje ya nchi. Kwa mfano, huduma hii ya upandikizaji uloto ikitolewa katika hospitali hii, itagharimu shilingi milioni 50 hadi 55 kwa mgonjwa mmoja,” amesema.Amesema hayo leo (Jumatano, Mei 10, 2023) wakati akizungumza na wananchi na watumishi wa hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma mara baada ya kuzindua huduma za kibingwa za upandikizaji wa uloto (Bone Marrow Transplant) hasa kwa watu wenye Seli Mundu (Sickle Cell).Waziri Mkuu amesema Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa inakuwa hospitali ya pili baada ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuzindua huduma hiyo ya upandikizaji wa uloto na hivyo, kuifanya kuwa miongoni mwa hospitali chache zinazotoa huduma hiyo katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na Kati.“Upandikizaji uloto unatoa nafuu kubwa sana kwa wagonjwa wa seli mundo kwani huwapunguzia kwa kiasi kikubwa maumivu na maambukizi ya mara kwa mara na wakati mwingine huwa sababu ya kupona kabisa kwa ugonjwa huu wa kudumu. Kutokana na nafuu hiyo, mgonjwa huweza kuishi maisha yenye ubora na kushiriki vema katika shughuli mbalimbali ikiwemo masomo”.Amesema uzinduzi wa huduma hiyo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa ni ushahidi tosha wa namna ambavyo Tanzania inapiga hatua kuboresha huduma za afya. “Huduma za namna hii kuendelea kutolewa katika hospitali zetu si jambo dogo, na hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa huduma kama hizi zinapatikana katika nchi chache sana kwenye bara la Afrika.”Katika hatua nyingine, Waziri Ummy amesema wizara hiyo inaangalia uwezekano wa kuipandisha hadhi hospitali hiyo ili iwe hospitali ya Taifa badala ya kuendelea kubakia kuwa ya kanda. “Tumeanza kujenga kituo cha kutoa tiba ya kansa na pia tunataka tujenge kituo cha umahiri cha matibabu ya moyo ili kuimarisha utoaji wa huduma kwenye hospitali yetu.”Naye Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika alimweleza Waziri Mkuu kwamba tangu Januari 19, mwaka huu hadi leo, wamefanikiwa kupandikiza uloto kwa watoto watatu na wote wanaendelea vizuri. “Watoto wawili wanatoka kijiji jirani cha Mapinduzi na mmoja anatoka eneo la Area D hapahapa Dodoma.” Alisema kufanyika kwa upandikizaji wa uloto kwenye hospitali hiyo, kumeifanya Tanzania iwe miongoni mwa nchi saba zinazotoa huduma hiyo barani Afrika. Alizitaja nchi nyingine zinazotoa huduma hiyo kuwa ni Algeria, Afrika ya Kusini, Misri, Morocco, Nigeria na Tunisia. “Kwa mantiki hiyo, Tanzania inakuwa nchi ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kuanza kutoa huduma hiyo.”Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Rosemary Senyamule amewapongeza watumishi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kazi nzuri wanayofanya ya  kuhudumia wagongwa na ameishukuru Serikali ya Awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuimarisha huduma katika sekta ya afya na kuwasogezea wananchi huduma kwa karibu katika Mkoa wa Dodoma.Aidha ,Senyamule ametoa ahadi ya kuendelea kusimamia huduma bora katika majengo yote yanayo jengwa ndani ya Mkoa na kuhakikisha  miradi hiyo inaisha kwa wakati ili kutekeleza dhamira ya fedha zilizo tolewa na serikali."Nimpongeze Mkurugenzi wa Hospitali hii ya Benjamin Mkapa imekuwa sifa katika nchi yetu ya Tanzania  wanakuja watu kutoka Mikoa mbalimbali lakini kinacho shanganza zaidi watu wanatoka Mkoa wa Dar-es-Salaam kuja kupata huduma huku "Kufuatia uzinduzi wa leo uliofanywa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Tanzania inakuwa moja kati ya nchi saba zinazotoa huduma hiyo barani Afrika.









Seen by Chindiye Happy at 19:35









Enter



















Write to Chindiye Happy














Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.