SERIKALI YAANZA UJENZI WA DARAJA LA CHIPOGORO BARABARA YA DODOMA IRINGA KWA GHARAMA YA SHILINGI MILIONI 601
Serikali kupitia Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) wameanza ujenzi wa daraja la Chipogoro Wilayani Mpwapwa katika barabara ya Dodoma Iringa litakalogharimu kiasi cha shilingi milioni 601 ambapo linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge katikati ya wiki hii amefanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ambao unatajwa kuwa wa manufaa makubwa kwa wananchi wa kijiji cha chipogoro, vijiji vya jirani na watumiaji wa barabara ya Dodoma Iringa. Jiografia ya eneo hilo linatuamisha maji mengi na kusababisha mafuriko nyakati za misimu ya mvua jambo ambalo lilihitaji kuwa na daraja litakalowezesha maji kupita yasituame.
Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa
Anuani ya Posta: 914 DODOMA
Simu: +255 26 232 4343/232
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz
Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.