• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

VIJANA WAASWA KUFANYA BIDII KATIKA KUYAFIKIA MALENGO NA NDOTO ZAO

Imetumwa : July 8th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Serikali inatamani kuwa na vijana wanaojitambua, wenye dira, malengo na ndoto za maisha yao pia wenye kufanya bidii katika kuyafikia malengo hayo. Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipohudhuria hafla ya uzinduzi wa mafunzo ya ufundi stadi na ugawaji wa vifaa iliyofanyika kwenye ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Chamwino Jijini Dodoma Julai 08, 2025.

Mhe. Senyamule ameyasema hayo kwa vijana wanaokwenda kuanza mafunzo ya ufundi stadi katika fani mbalimbali chini ya udhamini wa ‘World Vision Tanzania’ na Taasisi ya ‘Tanzania Home Economics Association’ (TAHEA) ambazo kwa pamoja zinatekeleza Mradi wa Vijana Balehe unaolenga kuongeza utambuzi wa masuala ya Afya ya uzazi kwa vijana balehe wa Kike na Kiume (AHADI)

“Tunatamani kama Serikali tuwe na vijana wanaojitambua ambao wana dira, ndoto za maisha yao, malengo, lakini wanafanya bidii kuyafikia hayo malengo. Nyinyi mmepata bahati ya kusikia na kuambiwa kwa hiyo bahati hiyo muitumie, hiyo elimu huko zamani haikuwepo, watu walikua wanakwenda kama vipofu nyinyi mnakwenda kama werevu na wenye maarifa, tumieni vizuri elimu zote ambazo mmepewa”. Mhe. Senyamule.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa TAHEA Bi. Lediana Mng’ong’o amesema wamekabidhi zawadi kwa vijana wawili waliohitimu mafunzo ya ufundi stadi kwa upande wa Upishi ambaye amepewa vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi 2,000,000 na aliyehitimu kwa upande wa urembo ambaye nae amepatiwa vifaa vyenye thamani ya shilingi 2,000,000 ili wakatimize ndoto zao.

Aidha, Mhamasishaji wa vijana walio kwenye mradi huo Bi. Scholastika Senga, amesema Vijana waliopewa zawadi kwenye hafla hiyo walionesha moyo wa kujituma kuanzia mwanzo wa mradi hadi mwisho hivyo wamepatiwa zawadi ili kutoa motisha kwa vijana wengine wanaoingia kwenye mafunzo stadi chini ya mradi huo.

Mradi wa AHADI unatekelezwa kwenye majiji ya Dar es salaam na Dodoma kuanzia Aprili 2024 hadi March 2029 ukilenga kuongeza utambuzi wa masuala ya afya ya uzazi na kuwawezesha kiuchumi Vijana Balehe wenye umri wa miaka 10-24 ambapo Mkoani hapa unatekelezwa katika Kata 12 za Chamwino, Nkuhungu, Mnadani, Msalato, Mkonze, Nzuguni, Kizota, Nala, Kikuyu Kusini, Kikuyu Kaskazini, Chang’ombe na Makole


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • VIJANA WAASWA KUFANYA BIDII KATIKA KUYAFIKIA MALENGO NA NDOTO ZAO

    July 08, 2025
  • HEKIMA ZA WAZEE KUSAIDIA KUDUMISHA AMANI YA NCHI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025

    July 08, 2025
  • RC SENYAMULE AZINDUA NYUMBA YA MWALIMU YA 02 KWA 01 KONDOA

    July 01, 2025
  • RAIS DKT. SAMIA ASISITIZA KUIMARISHWA KWA KILIMO ILI KUJIHAKIKISHIA USALAMA WA CHAKULA

    June 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.