• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Msaada
      • TEHAMA
      • Huduma za Sheria
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Manispaa ya Dodoma
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • Halmashauri ya Manispaa Dodoma
  • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAZIRI JAFO ATOA MAAGIZO MAZITO KWA MARAS, MADED NA MAAFISA MAWASILIANO WA SERIKALI

Imetumwa : March 17th, 2018

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo ametoa agizo kwa Ofisi za Mikoa na Halmashauri zote nchini kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa kwa vitengo vya Mawasiliano ili viweze kutekeleza majukumu yake.

Mhe. Jafo ametoa agizo hilo Jijini Arusha alipokuwa akifunga Kikao Kazi cha 14 cha Maafisa Mawasiliano Serikalini uliohudhuriwa na Maafisa Mawasiliano 300 kutoka katika Taasisi, Idara na Wakala wa Serikali, Mikoa, Majiji, Miji na Halmashauri zote nchini.


“Kuanzia mwaka ujao wa bajeti Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri, Majiji, Manispaa na Miji waweke kipaumbele kwa kutenga fedha za kununua vifaa muhimu kwa ajili ya Maafisa Habari na Mawasiliano ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo,” alisema Mhe. Jafo.

Vile vile ameagiza Maafisa Habari wapewe ushirikiano wa kutosha na Wakuu wa Idara kwa kuwapa taarifa na takwimu za idara zao ili kuwawezesha Maafisa hao kutoa taarifa muhimu za Serikali kwa vyombo vya habari na wananchi kwa wakati na bila vikwazo.

Aidha, amewataka Viongozi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutambuua kuwa Afisa Habari ndiye Mtendaji Mkuu katika masuala ya uandaaji wa habari, hivyo ni muhimu Maafisa hao kuingia katika vikao mbalimbali ili wapate uelewa wa masuala mbalimbali ya kimaamuzi yanayofanywa na uongozi.


Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Susan Mlawi amesema mada mbalimbali zimetolewa kwa lengo la kuwajengea uwezo Maafisa hao, ambapo miongoni mwa mada hizo ni pamoja na umuhimu wa Mawasiliano ya kimkakati katika kuisemea Serikali na tathmini ya utendaji katika mwaka 2017, maadili ya usalama katika kazi ya kuitangaza na kuisemea Serikali pamoja na wajibu wa Maafisa Habari katika mkakati wa kitaifa wa kupambana na maafa.

Nae, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo amesema ofisi yake itashirikiana na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kuhakikisha maazimio yote yaliyoafikiwa katika mkutano huo yanatekelezwa katika vitengo vyote vya Mawasiliano vya Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha.

Mkutano wa Maafisa Mawasiliano Serikalini unafanyika kila mwaka, ambapo kwa mwaka huu unafanyika kwa mara ya 14. Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Chama cha Maafisa Mawasiliano
 

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA KWENYE HALMASHAURI YA MANISPAA YA DODOMA March 27, 2018
  • TANGAZO LA AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPWAPWA March 27, 2018
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KWENYE HALMASHAURI YA WILAYA YA BAHI March 27, 2018
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KWENYE HALMASHAURI YA MJI KONDOA March 27, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RAIS MAGUFULI MGENI RASMI SHEREHE ZA MIAKA 54 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

    April 21, 2018
  • TBL KUJENGA KIWANDA KIPYA CHA BIA MKOANI DODOMA

    March 19, 2018
  • WAZIRI JAFO ATOA MAAGIZO MAZITO KWA MARAS, MADED NA MAAFISA MAWASILIANO WA SERIKALI

    March 17, 2018
  • RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA RELI YA KISASA KIPANDE CHA MOROGORO - DODOMA MAKUTUPORA

    March 14, 2018
  • Tazama Zote

Video

RAIS MAGUFULI MGENI RASMI SHEREHE ZA MUUNGANO
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Barabara ya Nyerere

    Anuani ya Posta: 914 Dododma

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.