• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

‘BASKET FUND’ YASAIDIA KUPUNGUZA VIFO VYA UZAZI MKOA WA DODOMA

Imetumwa : July 21st, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Mkoa wa Dodoma umefanikiwa kupunguza vifo vya Mama na watoto wachanga wakati wa kujifungua kutokana na uboreshaji mkubwa unaofanyika kwenye sekta ya Afya hususan kupitia msaada unaotolewa na Serikali ya Kanada nchini Tanzania kupitia Mfuko wa ‘Basket’ unaolenga kuboresha huduma za Afya ya uzazi.

Hayo yamebainishwa Julai 21, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri alipokua akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa ziara ya Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Kanada Mhe. Randeep Sarai katika Kituo cha Afya cha Makole Jijini humu.

“Malengo ya nchi ni kupunguza vifo wakati wa kujifungua kutoka 566 kwa vizazi hai 100,000 na hapa Dodoma  tumeona mabadiliko makubwa, kwa mwaka uliopita ambapo tulisajili vifo 75 kutoka vizazi hai 100,000 na 58 kutoka mwezi Januari mpaka sasa ambapo ni matokeo ya Mfuko huu”.

Aidha, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Thomas Rutachunzibwa, amesema kupitia ‘Basket fund’, walipokea shilingi Milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa majengo ya kutolea huduma za uzazi lakini bado hayakidhi ongezeko la wagonjwa hivyo, wameanza mradi wa ujenzi wa jengo la ghorofa nne ambapo wameomba msaada ili kulikamilisha kwa haraka.

Awali, akitoa taarifa fupi ya matumizi ya fedha za Mfuko zilizotolewa kwenye Kituo hicho , Mganga Mfawidhi wa Kituo Revocatus Baltazary, amesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, kituo kilipokea shilingi Milioni 638 sawa na Dola 244 ambapo 35% ilitumika kununua dawa, kukarabati chumba cha dawa, maabara na jengo la kuhifadhia vifaa vya kitabibu.

Vilevile, 65% ya fedha hizo pia ilitumika kuboresha huduma mbalimbali kama vile mafunzo kwa watoa huduma za afya, kusaidia huduma za lishe, huduma za uzazi wa Mpango pamoja na kuboresha huduma za Mkoba za ndani na nje.

Ziara ya Kiongozi huyo, inalenga kuangalia miradi ya Afya inayotekelezwa Nchini, hasa inayofadhiliwa na Serikali ya Kanada kupitia Mfuko wa ‘Basket’ inavyotoa huduma kwa wananchi, kwani Kanada ni moja ya wachangiaji wakubwa nchini kwenye sekta ya afya na Kituo cha Makole Mkoani hapa kinanufaika na Mfuko huo.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MRADI WA ‘KOFFI’ WATOA DOLA BILIONI 2.455 KUBORESHA HUDUMA ZA UZAZI NA MTOTO DODOMA

    August 21, 2025
  • WANANCHI NA WADAU WAASWA KUCHAGIZA UTALII - DODOMA

    August 21, 2025
  • WADAU WAASWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA JAMII DHIDI YA MAJANGA

    August 19, 2025
  • WAFANYABIASHARA WA MKOA WA DODOMA WATANGAZIWA FURSA ZA BIASHARA NCHINI INDONESIA

    August 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.