• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

BBT KULETA MAPINDUZI MAKUBWA YA KILIMO NA AJIRA NCHINI

Imetumwa : August 22nd, 2024

Miradi ya umwagiliaji inatarajiwa kuleta Mapinduzi makubwa katika sekta ya Kilimo nchini na kuzalisha ajira kwa wingi hasa kwa vijana. Hayo yamebainishwa wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Jenga Kesho iliyobora (Building a Better Tomorrow, BBT) katika Kijiji cha Mlazo Kata ya Ndogowe, Wilaya ya Chamwino.

Mradi huo uliozinduliwa Agosti 22, 2024 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philip Isdor Mpango, unalenga vijana kuingia kwenye kilimo cha kisasa chenye thamani na tija.

"Hili ni jambo la kimapinduzi la kubadilisha Taifa. Hapa Dodoma tumepewa hazina kubwa sana ya maji chini ya ardhi. Kupitia miradi hii ya Kilimo cha umwagiliaji, Dodoma hakuna tena njaa, zile salamu za njaa hazitakuwepo tena kwani chakula kitakua kingi na kingine tutauza" Amesema Mhe. Dkt Mpango.

Mradi huo uliopewa jina la Dkt Samia Suluhu Hassan, unaotekelezwa kwenye eneo la ekari 11,000 utahusisha vijana 420 kutoka mikoa mbalimbali nchini huku vijana 50 wakiwa ni wazawa wa eneo hilo. Mpaka sasa ujenzi wa Miundombinu ya umwagiliaji imefikia 35% ambayo inagharimu shilingi Bilioni 21.6

Mara baada ya uzinduzi huo, Makamu wa Rais alifanya Mkutano wa hadhara na wananchi wa eneo la Mpwayungu katika Wilaya hiyo ambapo ametoa maelekezo mbalimbali ikiwemo wafugaji wa eneo la Mradi watengewe eneo la malisho ili kuzuia kuingiza Mifugo kwenye eneo hilo.

Aidha, ametoa maelekezo kadhaa kama kujengwa kwa kituo cha Afya katika eneo la Mradi, TANROADS waboreshe Barabara kutoka Mpunguzi mpaka kwenye eneo la Mradi yenye urefu wa Km 100 ili kupitia Mradi huo, Barabara hiyo itawezesha Utalii kwenye mbuga ya Ruaha.

Mhe. Dkt. Mpango, amehitimisha ziara ya kikazi ya siku nne katika Mkoa wa Dodoma kwa kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa kwenye Wilaya Sita za Mkoa wa Dodoma kwa fedha kutoka Serikali kuu ikiwa na lengo la kuboresha huduma kwa wananchi. Miradi hiyo ni ile ya sekta za Elimu, afya, maji, kilimo, n.k



#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu













ReplyForward


Add reaction










Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.