• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

BILIONI 4.6 KUIBADILISHA RANCHI YA KONGWA

Imetumwa : March 15th, 2023

Serikali imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 4.6 kwa ajili ya kufanya maboresho makubwa katika ranchi ya Kongwa ikiwa ni pamoja na ununuzi wa mbegu bora za ng’ombe, uchimbaji wa visima na ununuzi wa matrekta.

Hayo yameainishwa na Bw. Elisa Binamungu Meneja wa Ranchi ya Kongwa wakati akisoma taarifa ya utendaji wa shamba la mifugo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua shamba la mifugo la NARCO – Kongwa ili kujionea maendeleo ya shamba na shughuli za ufugaji.

Bw. Binamungu amesema Serikali imeongeza uzalishaji wa nyama ya ng’ombe, ambapo ranchi ina ukubwa wa hekta 38,000 zenye uwezo wa kuweka uniti za mifugo 25,000.

“Eneo hili limegawanywa katika sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza ina jumla ya uniti za mifugo 12,427 na sehemu ya pili ina uniti za mifugo 16,897” Amesema Binamungu.

Akizungumza na wafanyakazi na wananchi wanaozunguka eneo la ranchi hiyo, Mhe. Senyamule amesema tunapoongelea mifugo tunaongelea uchumi wetu na kusisitiza kuwa Tanzania ni nchi ya pili barani Afrika kwa wingi wa mifugo ikitanguliwa na Ethiopia.

“Sisi tuna mifugo mingi sana ila mazao haya ya mifugo na nyama hayauziki nje kwa kiasi kikubwa, dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuweka msukumo Madhubuti katika eneo hili kwa kuwa lipo kundi kubwa linalotegemea mifugo” Senyamule amesisitiza.

Amesema, eneo la Kongwa lipo kimkakati hivyo menejimenti ya shamba hilo itumie fursa hiyo kuuza bidhaa zake na kujitangaza ipasavyo ili waweze kunufaika na uwepo wa barabara kuu.

“Serikali imetoa fedha nyingi ili kurejesha shamba hili katika hali yake ya ubora wajuu zaidi, tumieni fursa hii pia kutangaza shamba hili, wengi hawalifahamu. Nitoe rai kwenu kuendelea pia kuwa na mahusiano mazuri na jamii inayowazunguka ili wawe walinzi namba moja wa shamba hili” Senyamule amesisitiza.

Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Bw. White Zuberi amesema kuwa ranchi ya Kongwa ni muhimu katika kuimarisha uchumi wa Taifa na wana Kongwa kwa ujumla.

Ranchi ya Kongwa ni miongoni mwa Ranchi kongwe za Taifa na ipo katika Mkoa wa Dodoma, Wilaya ya Kongwa na kata ya Mtanana. Ranchi hii ndio ya kwanza kuanzishwa na ilianza wakati wa mkoloni

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.