• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DKT. BITEKO AZINDUA MRADI WA UMEME KILOVOTI 400 KUTOKA CHALINZE HADI DODOMA

Imetumwa : December 11th, 2024

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko, leo Desemba 11, 2024, amezindua mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Chalinze Mkoa wa Pwani hadi Dodoma unaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 513 sambamba na kuweka jiwe la msingi katika mradi huo.

Hafla hiyo imefanyika katika eneo la Zuzu Jijini Dodoma, ambapo mradi huo unalenga kuongeza uzalishaji wa umeme pamoja na upatikanaji wake kwa uhakika, ikiwa ni pamoja na ziada ya kuuza nchi jirani.

“Tupo mbioni kuhakikisha kuwa kila aliye jirani yetu kwa nchi zote zinazotuzunguka tunaziunganisha na umeme na njia za kupitisha umeme.Tumeshajiunga na Burundi, Rwanda, Kenya, sasa tunakwenda Zambia baadae tutajiunga na Malawi. Nia yetu ni kwamba umeme tulionao ,usiwe tu tunasema tuna umeme wa kutosha wakati tumeacha kufanya biashara na wenzetu.” Dkt Biteko

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga (MB), amesema Tanzania inategemewa na nchi za Mashariki mwa Afrika kwa mambo makubwa mawili ikiwemo miradi mikubwa ya uzalishaji umeme inayoendelea, lakini pia kwa miradi ya usafirishaji umeme ambayo inafanyika na inatambuliwa na nchi jirani.

Aidha,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amesema Mhe. Rais amewezesha vijiji vyote 564 vya Mkoa wa Dodoma kufikiwa na huduma ya umeme ambapo kwa sasa vijiji 22 vipo kwenye hatua za ukamilishaji lakini vijiji vingine vyote 542 umeme umeshafika na wananchi wanafurahia kufanya shughuli za kiuchumi kupitia matumizi ya nishati hiyo.

Katika hatua nyingine,Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga amesema mradi huu umekusudia kusafirisha umeme utakaozalishwa kwenye bwawa la Mwalimu Julius Nyerere ambao una ukubwa wa Megawati 2115 na kuingiza umeme huo kwenye gridi ya Taifa.

Ameongeza kuwa, hali ya upatikanaji wa umeme Nchini imeendelea kuimarika kutokana na uzalishaji wa umeme kukidhi mahitaji ambayo yameendelea kukua kwa kasi na kufikia Megawati 1888.72 ambayo yalifikiwa tarehe 26/11/2024 saa 2 usiku hali ambayo imechangiwa na kuunganishwa kwa mitambo mitano kutoka bwawa la Julius Nyerere kuingia katika gridi ya Taifa.


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu        

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.