• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TAASISI ZA KITAFITI TIBA ASILI ZASISITIZWA UFANISI WA VIWANGO VYA KIMATAIFA

Imetumwa : August 29th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Msisitizo umetolewa kwa Taasisi za Kitafiti, Vyuo Vikuu na Maabara kuendelea kufanya kazi za kisayansi ili kuboresha ubora, usalama na ufanisi wa dawa za tiba asili kwa lengo la kuipeleka sekta ya dawa za asili kwenye viwango vya Kimataifa.

Hayo yamebainishwa katika hotuba ya Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Khatibu Kazungu alipokua akihutubia siku ya kilele cha Wiki ya Tiba Asili kilichofanyika Agosti 29, 2025 katika Viwanja vya Bustani ya mapumziko Chinangali Jijini Dodoma.

“Taasisi za utafiti, Vyuo Vikuu na Maabara, endeleeni kufanya kazi za kisayansi ili kuboresha ubora, usalama na ufanisi wa dawa za tiba asili, lengo letu ni ili sekta hii tuweze kuipeleka katika viwango vya watu wa Kimataifa, uimarishaji wa viwanda na ushirikishwaji wa Wadau pia ufanyike ili kuongeza ubora na ushindani wa ndani na nje ya nchi”.

Aidha, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Bw. Ismail Rumatila amesema Shirika la Afya Duniani (WHO) linatoa kipaumbele kwenye huduma za tiba asili katika nchi wanachama kwani zimeendelea kufadhiliwa na kupewa kipaumbele hivyo Wizara yake kupitia idara ya Tiba asili imeandaa wiki hiyo kwa kuzingatia ufanisi na ubora wa hali ya juu.

Vile vile, Mganga Mkuu wa Serikali Grace Maghembe amesema kwa sasa dawa za tiba asili zimefanyiwa tafiti na zinatumika ndani ya Hospitali takribani 14 ambapo sasa mgonjwa ana uwezo wa kuchagua aina ya dawa ikiwa ni asili au za kisasa baada ya kufanyiwa uchunguzi na mganga na huduma hiyo inapatikana kwenye madirisha ya dawa.

Hata hivyo, Mwakilishi wa Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI anayehusika na masuala ya Afya Bw. Zuber Abdallah amesema katika kuhakikisha huduma za tiba asili zinatolewa kwa viwango bora, Serikali imechukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha huduma hizo zinakua endelevu lakini pia zina akisi mahitaji halisi ya jamii lakini pia ubora na ufanisi.

Wiki ya Tiba Asili ilianza kuadhimishwa takribani miaka 23 iliyopita ambapo ni matokeo ya kikao cha Wakuu wa nchi waliokaa Jijini Lilongwe nchini Malawi na kuangalia ni namna gani Bara la Afrika linaweza kutoa kipaumbele kwenye matumizi ya tiba asili na tiba mbadala kwani 80% ya wananchi wake wanatumia tiba mbadala.

Kauli mbiu: “Tuimarishe Huduma za Tiba Asili Zenye Ushahidi wa Kisayansi”

 #dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • TAASISI ZA KITAFITI TIBA ASILI ZASISITIZWA UFANISI WA VIWANGO VYA KIMATAIFA

    August 29, 2025
  • RC SENYAMULE APUNGUZA KERO ZA ARDHI KWA KIWANGO KIKUBWA MKOA WA DODOMA

    August 29, 2025
  • VIKUNDI 308 KUNEEMEKA NA BILIONI 3.6 ZA MIKOPO YA 10% DODOMA

    August 28, 2025
  • WATUMISHI WAASWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA KAZI

    August 26, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.