• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

VIKUNDI 308 KUNEEMEKA NA BILIONI 3.6 ZA MIKOPO YA 10% DODOMA

Imetumwa : August 28th, 2025

Na. Sizah Kangalawe

Habari – Dodoma RS

Benki washirika (NMB na CRDB) wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika utoaji mikopo ya 10% ya mapato ya ndani, wametakiwa kuhakikisha wanakamilisha hatua zao kwa wakati na uharaka ili iwafikie walengwa kwa muda uliopangwa.


Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa hafla ya uzinduzi wa utoaji mikopo ya 10% kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu, iliyofanyika Agosti 28, 2025 katika viwanja vya 'Nyerere Square' jijini Dodoma.


"Benki zote mbili, nyie ni washirika katika utoaji wa mikopo hii, pamoja na vigezo mnavyovisimamia naomba muwe msaada mkubwa kwa wananchi hawa wapate mikopo hii kwa haraka, ni kiu yao kuona ahadi aliyotoa Rais wao inawafikia kwa wakati," amesema Senyamule.


Pia Mhe. Senyamule ametumia fursa hiyo kuwaasa wanufaika wa mikopo hiyo kuitumia vyema na kuepukana na mkono wa sheria pindi watakapokwenda kinyume na mikataba yao.


"Napenda kuwakumbusha kuwa mikopo hii siyo zawadi bali ni mikopo nafuu isiyo na riba, ni vema mkaitumia vizuri na kuirejesha kwa wakati kama mlivyosaini mikataba yenu ili na wengine waweze kunufaika na fursa hii. Binafsi nisingependa kuona mwanakikundi yeyote anafikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa kushindwa au kukwepa kurejesha mkopo," ameongeza Senyamule.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri amesema wilaya yake ipo tayari kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha jambo hilo.


"Niwaombe wadau ambao mtapewa mikopo hii leo, mkawe mabalozi wazuri, mkatumie fedha vizuri, mkafanye marejesho kwa wakati ili muwaondoshe hofu mabenki. Hizi changamoto za leseni ya biashara sisi tupo tayari kuwa na timu ya pamoja na watu wa halmashauri ili wakija ambao hawana washughulikiwe kwa haraka na wapatiwe mkopo wasikwame," amesema Shekimweri.


Akitoa taarifa za mikopo hiyo, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Dkt. Fredrick Sagamiko amesema Bilioni 3,617,857,852.00 zitakopeshwa kwa vikundi 308 kupitia benki za NMB na CRDB.


Fedha hizo zimekusanywa kupitia mapato ya ndani kwa miaka miwili, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Tanzania kuwa halmashauri zote Nchini zitenge 10% ya mapato yao na kuzikopesha bila riba kupitia vikundi vya uzalishaji vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu.


Hata hivyo Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kushirikiana na VETA Dodoma wameandaa mafunzo kwa vijana watakaonufaika na mikopo ya bajaji na bodaboda, ili kukidhi vigezo vya kuendesha vyombo hivyo ikiwemo kuwa na leseni za udereva. Mafunzo hayo yatatolewa kwa gharama nafuu na yanatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi Septemba.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC SENYAMULE APUNGUZA KERO ZA ARDHI KWA KIWANGO KIKUBWA MKOA WA DODOMA

    August 29, 2025
  • VIKUNDI 308 KUNEEMEKA NA BILIONI 3.6 ZA MIKOPO YA 10% DODOMA

    August 28, 2025
  • WATUMISHI WAASWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA KAZI

    August 26, 2025
  • MRADI WA ‘KOFFI’ WATOA DOLA BILIONI 2.455 KUBORESHA HUDUMA ZA UZAZI NA MTOTO DODOMA

    August 21, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.