• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DODOMA KUFUNGUA BARABARA KUELEKEA HIFADHI YA TAIFA RUAHA KUKUZA UTALII WA NDANI

Imetumwa : June 10th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari - DODOMA RS

Mkoa wa Dodoma upo kwenye Mpango Mkakati wa kukuza sekta ya Utalii kwa kujenga barabara na daraja kwenye mpaka wa Mkoa huo na Iringa uliopo katika Kijiji cha Ilangali Wilaya ya Chamwino litakalotumika kuunganisha wananchi wa Kata ya Manda na Hifadhi ya Taifa Ruaha ambapo itatengeneza fursa za kibiashara kwa Watalii watakaokwenda kwenye hifadhi hiyo kupitia Mkoani hapa.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipofanya ziara ya kikazi kwenye eneo la mpaka lililopo kwenye Kijiji cha Ilangali, Kata ya Manda katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Juni 10, 2025.

"Tulianza kutengeneza Mpango Mkakati wa kukuza Utalii kwenye Mkoa wetu wa Dodoma ambapo kivutio kikubwa Mbuga ya Ruaha ambayo inapakana na Mkoa wetu wa Dodoma, ambapo tunajenga barabara na daraja la kutuvusha hapo ili tuweze kufika Ruaha na kuwe na njia ya kupita hapa kuingia 'Ruaha National Park".

Mhe. Senyamule ameongeza kuwa hiyo ni fursa ya kuinua uchumi kwa wakazi wa Manda kupitia huduma watakazozitoa kwa wageni watakaokua wakielekea Mbugani hivyo ametoa shime kwa wakazi hao kujiandaa kutoa huduma mbalimbali kama malazi, bidhaa za utamaduni, vyakula na vitu vingine pindi barabara na daraja hilo vitakapokamilika.

Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja amewasilisha kero kubwa inayowakabili wakazi wa eneo hilo ambayo kuvamiwa na wanyama pori hususan Tembo ambao huharibu mazao na kutishia maisha yao hivyo amesema kujengwa kwa barabara na daraja eneo hilo kutapunguza kadhia hiyo na kutengeneza fursa kwa Wananchi hao.

Akijibu kero ya Tembo kuvamia Makazi ya watu, Afisa Mfawidhi kutoka Kituo cha TAWA Dodoma Bw. Prosper Kawishe amesema wameagiza vifaa vya kutosha kwa ajili ya kuwapatia vijana waliopata mafunzo ya kuwadhibiti Tembo hao ili wasiingie kwenye makazi na kuharibu mazao  au kuhatarisha maisha ya Wananchi na kipaumbele itakua Kijiji cha Ilangali.

Mbali na kutembelea eneo hilo la mpaka, Mhe. Senyamule ametembelea Mradi wa maji unaotekelezwa na Shirika la 'Water Mission' chini ya ufadhili wa Shirika la 'Charity Water'' katika Kijiji cha Manda unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi Milioni 790.7 ambao unatarajiwa kuwanufaisha wananchi 9,921 wa Kijiji hicho huku ukitarajiwa kukamilika June 30, 2025.

Ziara ya Mkuu wa Mkoa ilihitimishwa kwa kufanya Mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Manda ambapo walipata fursa ya kuwasilisha kero zao mbele ya Mhe. Senyamule na Wataalamu alioambatana nao ambapo majawabu ya kero hizo yalipatikana.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DODOMA YAENDELEA NA MAANDALIZI KUELEKEA SIKU YA KUPINGA DAWA YA KULEVYA DUNIANI

    June 12, 2025
  • VITUO VYA AFYA MSINGI MKOANI DODOMA VYAONGOZA MATUMIZI YA MFUMO WA ‘ GoTHOMIS’ KWA 98%

    June 12, 2025
  • DODOMA YAANZA KWA KISHINDO UMITASHUMTA - IRINGA

    June 10, 2025
  • DODOMA KUFUNGUA BARABARA KUELEKEA HIFADHI YA TAIFA RUAHA KUKUZA UTALII WA NDANI

    June 10, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.